Sunday, June 11, 2017

MAFANIKIO HAYAHITAJI KUOMBA RADHI, KUSHINDWA HAKUNA VISINGIZIO.

📖MAFANIKIO HAYAHITAJI KUOMBA RADHI, KUSHINDWA HAKUNA VISINGIZIO.

Ustahimilifu na akili iliyofunguka ni mahitaji ya kivitendo kwa muotajindoto wa leo. Wale ambao ni waoga wa mawazo mapya hushindwa kabla hawajaanza. Haijawahi kutokea wakati muafaka zaidi kwa waasisi  kushinda sasa. Kuna biashara nyingi zisizomithilika, dunia ya kifedha na kiviwanda kuumbwa tena upya na kuelekezwa sambamba na njia mpya zilizokuwa bora zaidi.

Katika kupanga kupata mgawo wako wa utajiri, usiruhusu mtu akushawishi kumdharau muotajindoto. Kuvishinda vigingi vikubwa katika hii dunia inayobadilika kila wakati, ni lazima uwe na roho ya waasisi wakubwa wa zamani ambao ndoto zao zimeupa ustaarabu kila kitu cha thamani uliyokuwa nacho, roho ambayo hutumikia mithili ya damu ya uhai wa jamii yetu-nafasi yako na yakwangu, kuendeleza na kutafuta soko la vipaji vyetu....... #Napolian Hill

Tusisahau, Columbus aliota juu ya Dunia isiyojulikana, akihatarisha maisha yake kwa uwepo wa dunia hiyo, na aliivumbua! Copernicus, mwana-elimu ya anga, aliota juu ya uwepo wa sayari nyingi, na hilo alilithibitisha! Baada ya kusherekea ushindi hakuna mtu aliyemshutumu hadharani kuwa aliyoyasema yalikuwa hayatekelezeki. Badala yake Dunia ilitoa heshima kubwa kwenye kaburi lake, hivyo kuthibitisha kwa mara nyingine tena kwamba, mafanikio hayahitaji kuomba radhi, kushindwa hakuna kisingizio.....

#Nice week end...
#Nice Sunday....
#Nice day...

Monday, April 10, 2017

AKUSHINDAE KUONGEA, MSHINDE KUNYAMAZA.

AKUSHINDAE KUONGEA, MSHINDE KUNYAMAZA.

MITHALI 11:12 Asiye na akili humdharau mwenziwe; Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza.

MITHALI 17:28 Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima; Akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu.

Changamoto kubwa tuliyonayo ni kwamba tunataka kuongea kila wakati, tunataka kujibu kila tunachokisikia, kila tunachokiona tunataka kukisemea kitu.

Kuna wakati tunasikia na kukutana na mambo ambayo kiuhalisia moyo unagoma kabisa kunyamaza, unatamani ujibu, unatamani uwaambie watu yale umefanyiwa, unatamani uelezee vile umeumizwa lakini kumbe si kila jambo linatakiwa kuongelewa.

Si kila ukionacho unatakiwa kukisemea kitu. Si kila usikiacho/uambiwacho ni lazima ujibu.

Si kila ufanyiwacho ni lazima umwambie kila mtu.

MUHUBIRI 3:1 Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.

Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona; Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena;

Ipo nguvu katika kunyamaza

Yapo mambo ambayo tunapaswa kuongea, kusema, lakini yapo mambo ambayo tunapaswa kunyamaza kwa ajili ya usalama wa Roho zetu.

Ni kweli kuna wakati unasemwa sana vibaya, unasingiziwa, unatukanwa nk nk, lakini ni lazima ukumbuke kwamba kuna mazingira ambayo hupaswi kujibizana hata kama umeumia kiasi gani.

Unajua ni kwanini?

Ukisemwa vibaya, ukitukanwa, ukidharauliwa lazima moyo utaghafilika, moyo ukighafilika lazima utakuwa na hasira na ghadhabu.

Ukiwa na hasira katu usitegemee kuwa utajadiliana na mtu kwa hekima.

Ukiongea utaongea katika uwepo wa hasira, ukijibu utajibu kulingana na kiwango cha hasira ulichonacho.

Sasa jiulize majibu yanayotoka kutokana na msukumo wa hasira huwa yanakuwaje?

AMOSI 5:3 Kwa ajili ya hayo mwenye busara atanyamaza kimya wakati kama huo; kwa kuwa ni wakati mbaya.

1 SAMWELI 25:1

Ni vyema sisi pia tukajifunza kusoma mazingira na nyakati na hali za watu zilivyo ili tujue ni wakati gani tujibu, tuongee nini na ni wakati gani tunyamaze

Kilinde kinywa, hakikisha haukiachi kinene mabaya – ZABURI 50:19.

Usipoteze marafiki na kuharibu mahusiano kwa ajili ya kinywa kibovu –MITHALI 11:9.

Ni vyema tukajifunza kujua ni neno gani tukitamka kwa wakati/hali/mazingira gani litakubaliwa – MITHALI 10:32.

ZABURI 19:14 – Bwana na akafanye maneno yetu yakapate kibali mbele zake MUNGU na mbele za wanadamu pia.

1SAMWELI 25:36

Umeumizwa, umekwazwa, umetukanwa, umedharauliwa, KATIKA MAZINGIRA YA HASIRA NA GHADHABU JITAHIDI KUNYAMAZA.

Monday, March 27, 2017

MLO KAMILI HASA KWA MAMA MJAMZITO ILA SOMA HII KWANI HATA WEWE ITAKUSAHIDIA..

MLO BORA KWA MAMA MJAMZITO.

Kwa ajili ya afya ya mama na mtoto ni muhimu sana mwanamke apate chakula bora. Ukosekanaji wa chakula bora kunaweza kukasababisha mtoto kuzaliwa kabla ya mda wake au na uzito mdogo ambao unaweza ukachangia katika kuzuia ukuaji wa ubongo na mwili kwa ujumla.

Na endapo mama mjamzito atakosa mlo bora uliombatana na protini anaweza akapata anaemia, infection, matatizo katika placenta, matatizo katika labor, c-section(kuzaa kwa upasuaji wakati wa kujifungua), kutokupona kwa haraka, matatizo katika kunyonyesha, toxemia na pre-eclempisa(haya ni magonjwa yanayosababishwa na maini kutoweza kufanya kazi yake vizuri

Hivyo ili kujenga afya ya mama na mtoto imeshauriwa ya kwamba mama mjamzito anatakiwa apate 100 grams za protein kwa siku.

Ifuatayo ni mlo kamili anaotakiwa apate mama mjamzito kila siku ya ili kuweza kupata afya bora:

1.Maziwa na vyakula vya jamii ya maziwa:
Glasi nne au zaidi ya maziwa ya aina yoyote pamoja na/au vyakula vyenye jamii ya maziwa kama jibini, mtindi,siagi, ice cream. Maziwa ni muhimu kwa protein, calcium, vitamins na virutubisho vingi. Vitasaidia ukuaji wa mifupa, misuli na nerves. Ni muhimu kwa damu yenye afya, kusaidia usingizi na kusawazisha mapigo ya moyo.

Mayai:
Mayai mawili kwa siku husaidia kuupa mwili protein, vitamins minerals na vitamin A ambayo itasaidia kuzuia infections.

Vyakula vyenye Protein
Serving mbili ya samaki, maini , kuku, nyama ya ngombe, mbuzi, kondoo au nguruwe, maharagwe au jibini. Kusaidia ujengaji mifupa, meno, misuli, ubongo na mwili kwa ujumla. Ukosekanaji wa protein ya kutosha kutasababisha kuchoka, uvimbe na kutojisikia kula au appetite ndogo.

Mboga za majani.
Spinach, cabbage, collard greends, mchicha, matembele. Mboga hizi ziwe fresh na zile zenye rangi ya kijani iliyokolea(hizi ndio zenye virutubisho vya kutosha).  Mboga hizi zitakupa Vitamin A na B, pia virutubisho vitakavyosaidia mwili kuabsorb protein ya kutosha, ukuaji wa mwili, na utengenezaji wa damu. Kutopata mboga za kutosha kunaweza sababisha mama kupata anemia.

Vyakula vyenye vitamin C.
Kipande kimoja au viwili vya machungwa au juisi ya ndimu, machungwa, nyanya. Vitamin C itasaidia uterus kuwa na nguvu ya kutosha ili kufanya kazi vizuri wakati wa labor, pia itasaidia kulinda mwili na infection na kusaidia kuabsorb iron kwenye mwili.

Maji ya kunywa.
Kunywa maji mengi ya kutosha. Maji huchangia kwa asilimia 75 ya uzito wa mtoto wako atakapozaliwa. Usipopata maji ya kutosha utaishiwa na nguvu kwa asilimia 20 na kupata matatizo ya dehydration na kichwa kuuma.

Tumia chumvi kiasi.
Chumvi  kusaidia kuzunguka kwa damu kutoka mwilini kwenda kwenye placenta. Kutopata chumvi ya kutosha kunaweza kusababisha miguu kuuma na uchovu.

Kwenye sehemu ya pili tutaongelea virutubisho kadhaa na umuhimu wake kwa mama mjamzito na mtoto. Ila kumbuka utumiaji wa chumvi kwa wingi una madhara kiafya.

MLO KAMILI HASA KWA MAMA MJAMZITO ILA SOMA HII KWANI HATA WEWE ITAKUSAHIDIA..

MLO BORA KWA MAMA MJAMZITO.

Kwa ajili ya afya ya mama na mtoto ni muhimu sana mwanamke apate chakula bora. Ukosekanaji wa chakula bora kunaweza kukasababisha mtoto kuzaliwa kabla ya mda wake au na uzito mdogo ambao unaweza ukachangia katika kuzuia ukuaji wa ubongo na mwili kwa ujumla.

Na endapo mama mjamzito atakosa mlo bora uliombatana na protini anaweza akapata anaemia, infection, matatizo katika placenta, matatizo katika labor, c-section(kuzaa kwa upasuaji wakati wa kujifungua), kutokupona kwa haraka, matatizo katika kunyonyesha, toxemia na pre-eclempisa(haya ni magonjwa yanayosababishwa na maini kutoweza kufanya kazi yake vizuri

Hivyo ili kujenga afya ya mama na mtoto imeshauriwa ya kwamba mama mjamzito anatakiwa apate 100 grams za protein kwa siku.

Ifuatayo ni mlo kamili anaotakiwa apate mama mjamzito kila siku ya ili kuweza kupata afya bora:

1.Maziwa na vyakula vya jamii ya maziwa:
Glasi nne au zaidi ya maziwa ya aina yoyote pamoja na/au vyakula vyenye jamii ya maziwa kama jibini, mtindi,siagi, ice cream. Maziwa ni muhimu kwa protein, calcium, vitamins na virutubisho vingi. Vitasaidia ukuaji wa mifupa, misuli na nerves. Ni muhimu kwa damu yenye afya, kusaidia usingizi na kusawazisha mapigo ya moyo.

Mayai:
Mayai mawili kwa siku husaidia kuupa mwili protein, vitamins minerals na vitamin A ambayo itasaidia kuzuia infections.

Vyakula vyenye Protein
Serving mbili ya samaki, maini , kuku, nyama ya ngombe, mbuzi, kondoo au nguruwe, maharagwe au jibini. Kusaidia ujengaji mifupa, meno, misuli, ubongo na mwili kwa ujumla. Ukosekanaji wa protein ya kutosha kutasababisha kuchoka, uvimbe na kutojisikia kula au appetite ndogo.

Mboga za majani.
Spinach, cabbage, collard greends, mchicha, matembele. Mboga hizi ziwe fresh na zile zenye rangi ya kijani iliyokolea(hizi ndio zenye virutubisho vya kutosha).  Mboga hizi zitakupa Vitamin A na B, pia virutubisho vitakavyosaidia mwili kuabsorb protein ya kutosha, ukuaji wa mwili, na utengenezaji wa damu. Kutopata mboga za kutosha kunaweza sababisha mama kupata anemia.

Vyakula vyenye vitamin C.
Kipande kimoja au viwili vya machungwa au juisi ya ndimu, machungwa, nyanya. Vitamin C itasaidia uterus kuwa na nguvu ya kutosha ili kufanya kazi vizuri wakati wa labor, pia itasaidia kulinda mwili na infection na kusaidia kuabsorb iron kwenye mwili.

Maji ya kunywa.
Kunywa maji mengi ya kutosha. Maji huchangia kwa asilimia 75 ya uzito wa mtoto wako atakapozaliwa. Usipopata maji ya kutosha utaishiwa na nguvu kwa asilimia 20 na kupata matatizo ya dehydration na kichwa kuuma.

Tumia chumvi kiasi.
Chumvi  kusaidia kuzunguka kwa damu kutoka mwilini kwenda kwenye placenta. Kutopata chumvi ya kutosha kunaweza kusababisha miguu kuuma na uchovu.

Kwenye sehemu ya pili tutaongelea virutubisho kadhaa na umuhimu wake kwa mama mjamzito na mtoto. Ila kumbuka utumiaji wa chumvi kwa wingi una madhara kiafya.

Friday, March 17, 2017

UKIENDELEA NA TABIA HIZI MAFANIKIO KWAKO YATAKUWA NI NDOTO

UKIENDELEA NA TABIA HIZI MAFANIKIO KWAKO YATAKUWA NI NDOTO.

Hasira za mafanikio zinatofautiana baina ya mtu mmoja na mwingine. Kama kweli unahitaji mafanikio ya kweli ni lazima uwe na hasira ya njaa kama aliyonayo simba. Miongoni mwetu ni watu wachache sana wanatambua hasira hii ya mafanikio, wengi wetu huchukulia mafanikio kwa sura ya kawaida sana na mwisho wa siku tunaishia kuwa maskini.

Binadamu ni kiumbe wa ajabu sana, nasema hivi ni kiwa na maana ya kwamba binadamu anapenda sana maisha ya kufanyiwa kila kitu, kwa mfano mtu anapenda umpikie chai, umuwekee kwenye chupa, umuwekee chai kwenye kikombe na umgorogee na sukari katika chai na ukishamfanyia yote hayo subiri anywe hiyo chai uone atakavoanza kulaamu utamskia anasema sukari imezidi au sukari hajikolea na lawama zingine nyingi, kitu cha kujiuliza je, mtu huyo alishindwa kuweka sukari mwenyewe kwenye chai yake ili jambo lolote likitokea akose wa kumlamu.

Mtu huyo huyo ukimuuliza unafanya biashara gani? Utamsikia anasema sifanyi biashara yeyote ile mi nipo tu, ukimuuliza kwanini haufanyi biashara yeyote tatizo nini? Atamsikia anakujibu tatizo mtaji huku akiamini kuwa mataji pekee katika biashara ni fedha. Ndugu msomaji wa makala hii hata uwe na fedha kiasi gani kama huna wazo kwa ajili ya matumizi ya fedha, hata ukipewa milioni mia moja leo hizo pesa zitaisha utajikuta mwisho wa siku huna hata mia mbovu. Watu wengi tunatazama mitaji kama fedha peke yake ukitazama katika msingi huo utazidi kulamu mpaka mwisho huku maisha yakiendelea kuwa magaumu.

Ngoja nikuibie siri mtaji unaweza ukaupata kwa kutumia ujuzi pamoja nguvu ulizonazo ili kutengeneza bidhaa au huduma zitazokufanya upate fedha. Kwa mfano Wewe mwenye elimu juu tekinologia ya habari na mawasiliano unaweza ukabili ujuzi wako kuwa bidhaa kwa kuwa fundi wa computer na kutengeza progamu mbalimbali. Swali la kujiuliza unaweza vipi kubadili ujuzi ulio nao kuwa bidhaa au huduma hapo ndipo wengi tunapofeli kwa sababu ni wavivu wa kufikiri.

Naendelea kumchambua binadamu ili uone ni jinsi gani tulivyokuwa na tabia za lawama. Binadamu huyo huyo utamkuta anaishi mazingira machafu ambayo yatasababisha muda wowote magonjwa ya mlipuko kutokea, ukimfuta binadamu huyo na kumuuliza unafikiri ni kwanini mazingira haya ni machafu, utamsikia jibu atakalokupa atakwambia tatizo ni serikali, binadamu huyohuyo utamkuta hana ajira ila ukimuuliza kwanini hauna ajira? Atakujibu tatizo ni serikali.

Kuna msanii mmoja wa hapa nchini aliwahi kuimba kwenye wimbo huku akiuliza serikali ni nini? Maana imekukuwa ikutupiwa lawama kwa kila kitu. Ndugu msomaji wa makala haya nakusihi na kukushauri pia kwa kile ambacho unaweza kukifanya usisubiri serikali ndio ukifanyie, kama unauwezo wa kufanya usafi katika eneo lako fanya usisubiri kuambiwa, maana tabia za bianadamu kwa asilimia kubwa wanasubiri kuambiwa fanya hiki fanya kile . UKisubiri kuambiwa maisha ya mafanikio kwa upande wako yatakuja kwa asilimia chache sana.

Kitu cha msingi ya kuzingatia ni kwamba tuache lawama sizisokuwa na msingi wowote, kwani lawama ulizonazo leo hata yule unayemlalamikia hakusikii na unazidi kuwa maskini tu. Jambo la msingi fanya kila kitu kwa moyo mmoja bila kusubiri mtu fulani akwambie ufanye. Daima tukumbuke usemi huu “ kila uonapo nyundo usifikiri kila tatizo ni msumari’’

Mafanikio ya kweli huja kwa mtu kujitambua yeye ni nani? Na ni kwanini upo hapo ulipo. Kuna usemi mmoja hivi wa kiswahili unasema kila binadamu ni mchungaji ,kama ndivo hivyo basi kama mimi leo nikiulizwa nimechunga nini, jibu langu litakuwa lipo wazi ya kwamba natumia muda mwingi kuwafunza watu ili kujua mbinu za kufanikiwa, je wewe mwenzangu unasoma makala hii endapo utaulizwa swali kama hilo utajibu nini? Tafakari kisha uone una thamani gani mbele ya watu wengine?.

Wednesday, March 15, 2017

WEWE NI MTOTO WA NGAPI KUZALIWA?

WEWE NI MTOTO WA NGAPI KUZALIWA? 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇 FAHAMU NGUVU ZAKO ZA KUZALIWA KWA UFUNUO WA ROHO MTAKATIFU

Kumb 33:1-9, Mwanzo 49:3-7, 1Kor 2:10
Kila mwanadamu aliyeumbwa na Mungu Aliye Hai, ameumbwa na nguvu maalumu kutoka mbinguni, ambayo ni mtaji wake maalumu; kiroho, kijamii na kiuchumi.
Mwanzo 49:3
Reubeni u mzaliwa wangu wa kwanza,nguvu zangu na malimbuko ya uwezo wangu. Umewapita wengine kwa ukuu na nguvu.

1. MZALIWA WA KWANZA KATIKA FAMILIA YOYOTE
i. Amebeba nguvu nyingi za familia.
ii. Amebeba Baraka za aina mbalimbali za wadogo zake.
iii. Amebeba nguvu ya upendo ndani ya familia.
iv. Mzaliwa wa kwanza ni lango, Zab 24:7-9, ambapo Baraka zote za familia kutoka mbinguni zinapitia kwake na kuwafikia wadogo zake wote.
v. Amebeba ustawi wa familia kiroho na kimwili.

2. MTOTO WA PILI KATIKA FAMILIA YOYOTE
i. Ni m’beba neno la uzima.
ii. Kipawa cha ualimu kinakaa vizuri sana ndani yake.
iii. Amepewa neno la uzima la kusaidia kanisa familia na nchi.

3. MTOTO WA TATU KATIKA FAMILIA YOYOTE:
i. Ni mtawala katika ulimwengu wa roho  na wa mwili.
ii. Ni mtunga sheria popote atakapokuwa anaishi, anasoma au anafanya kazi.
iii. Amepewa mamlaka ya kusimamia jamii, kuiongoza na kuitawala.
iv. Anafaa kuwa mwanasheria au kiongozi popote aendapo.

4. MTOTO WA NNE KATIKA FAMILIA YOYOTE
i. Amepewa neema ya kumiliki utajiri wa nchi.
ii. Kama akijitambua na kusimama katika zamu yake, ajue amepewa neema na nguvu ya kuutawala uchumi vizuri sana.
iii. Amepewa nguvu ya kumiliki utajiri wa mbingu na dunia.

5. MTOTO WA TANO KATIKA FAMILIA YOYOTE
i. Amepewa neema ya kushinda changamoto.
ii. Amepewa stamina ya kushindana na majaribu kwa asili.
iii. Amepewa neema ya kutumika na upako wa juu sana, kama akiokoka na kujitambua, na kusimama katika zamu yake.

6. MTOTO WA SITA KATIKA FAMILIA YOYOTE
Ni mtu wa ujuzi, na talanta.  Na Amepewa nguvu ya ubunifu wa pekee.

7. MTOTO WA SABA KATIKA FAMILIA YOYOTE
i. Amebeba uheri wa Mungu Mtakatifu.
ii. Yeye ni jubilee, yaani maachilio.
iii. Usithubutu kushindana naye maana hautafanikiwa.
iv. Ukimshitaki hauwezi kufanikiwa.
v. Anafaa kuwa mzee wa kanisa.
vi. Anafaa kuwa hakimu kama ataamua kuichukua taaluma hii.
vii. Ukipata kesi yoyote na akakusindikiza ni lazima utashinda, maana utu wake wa ndani ameumbiwa neema hii.

8. MTOTO WA NANE KATIKA FAMILIA YOYOTE
i. Amebeba nguvu ya utumishi.
ii. Amepewa neema ya kusaidia wengi kiuchumi, kiroho na kijamii, kama akijitambua na kusimama katika zamu yake.
iii. Akiokakoka na kuwa mtumishi kanisa lolote, atalisaidia sana kustawi, kwa kuwa ni mtu wa kutegemewa sana.
iv. Amepewa neema ya kuwa nguzo.
v. Ukimtambua katika kanisa lako na kumthamini, na kumtumia vizuri, utafanikiwa sana.

9. MTOTO WA TISA KATIKA FAMILIA YOYOTE
i. Ni m’beba karama.
ii. Akipokea kipawa anakitunza sana kwa muda mrefu.
iii. Amepewa nguvu ya umoja.
iv. Ni mtu anaweza kuinganisha jamii, nchi au familia na kuleta mshikamano.
v. Anafaa kuwa mwanasiasa endapo akijitambua na kusimama katika nafasi yake aliyokirimiwa na mungu.

10.  MTOTO WA KUMI KATIKA FAMILIA YOYOTE
i. Yeye ni msamaha.
ii. Amekirimiwa nguvu ya msamaha.
iii. Amepewa uwezo wa kusuluhisha migogoro kwa ufanisi wa hali ya juu sana.
iv. Anafaa kuwa mzee wa kanisa.

11.   MTOTO WA KUMI NA MOJA KATIKA FAMILIA YOYOTE
Ni faraja kwa familia.
Kuna wakati anapata tatizo la kukataliwa, lakini ni mvumilivu sana.
Mkikaa naye kwa upendo mtabarikiwa sana.
JIULIZE WEWE NI MTOTO WA NGAPI  NAJEE UNAITENDEA VYEMA NAFASI YAKO?

Monday, March 13, 2017

Mvua yaleta mafuriko jijini Dar

https://youtu.be/BHqVGLWoMkI

ACHA KUWA MVIVU MPENDWA SOMA HII

MVIVU

"Mtu yeyote anayekuambia juu ya hatari zilizoko kwenye njia yake kuelekea mafanikio anayoyataka, na anadai ndio sababu ya yeye kuacha kuchukua hatua kuelekea mafanikio, MTU HUYU NI MVIVU"
(Mithali 22:13).

"Mtu yeyote ALIYEFUNGA NDOA NA GODORO, anafanya kazi ya kugeuza mbavu zake, kama mlango unavyogeuka kwenye bawaba, MTU HUYU NI MVIVU"
(Mithali 26:14).

"Mtu anayependa kusukumwa sukumwa, kusimamiwa simamiwa, kuelekezwa elekezwa, kuambiwa ambiwa mambo ambayo alipaswa kujiambia, kujielekeza, kujisukuma, kujisimamia, MTU HUYU NI MVIVU"
(Mithali 6:6-8).

"Mtu asiyefikiri kuhusu kesho, na kuweka mikakati ya kuikabili hiyo kesho, anasubiri vitu vitokee bila mipango na maandalizi, MTU HUYU NI MVIVU"
(Mithali 6:6-8).

"Mtu yeyote ambaye mambo yake yako shaghalabaghala, hayana mipangilio, hayana unadhifu, uzuri na ubora, MTU HUYU NI MVIVU"
(Mithali 24:30-34).

"Mtu yeyote anayeuhurumia mwili wake, na anapenda kujihurumia hurumia, badala ya kuutesa mwili na matakwa yake ya muda mfupi, MTU HUYU NI MVIVU"
(Mithali 20:4).

Mtu yeyote ambaye ukijaribu kumulekeza yampasayo ili afanikiwe, anajitia mjuaji na anakupa sababu nyingi za kwanini haiwezekani, badala ya kwanini aweze, MTU HUYU NI MVIVU
(Mithali 26:16). 

NAIAMURU ROHO CHAFU YA UVIVU IKUTOKE KWA JINA LA YESU.

Saturday, March 11, 2017

MPIRA UMEKWISHA YANGA 1 ZANACO 1 HII NDIYO TATHIMINI KWA TIMU YANGU DAR- YOUNG AFRICAN

MPIRA UMEKWISHA YANGA 1 ZANACO 1
TATHIMINI KWA YANGA SC
George Lwandamina kaianza vyema mechi kwa hesabu za kimbinu na kiufundi. Licha ya kasi na matumizi makubwa ya nguvu aliwaweza kwenye marking na kuwatoa mchezoni kwa kuwatumia Yondani , Zulu , Kamusoko na Ngoma .
Timu imetengeneza nafasi nyingi za kufunga sema utulivu wa forward line ya Yanga kwenye finishing ilikuwa tatizo ukiacha nafasi moja waliyoipata na Msuva kufunga bao dakika ya 39. Ni goli lililotafutwa vizuri kimbinu kazi ikianzia kwa Ngoma akirudi chini kama Play maker na kumpasia Zulu wing ya kulia ambaye kwa utulivu mkubwa anamtengea Msuva ndani ya 18 na yeye akionesha kuwa yupo matured anatengeneza goli zuri.
Nini kimewafanya Yanga kushindwa kulinda goli?
Kwa macho mepesi unaweza mtupia lawama kocha kwa mabadiliko aliyoyafanya kwa kuwatoa Ngoma na Kamusoko na kuwaingia Emanuel Martini na Juma Mahadhi na ndipo Zanaco walipoanza kuja kwa kasi na kutengeneza goli.
Kwanza kabisa ni lazima tukubali jambo moja kabla ya kumtupia lawama kocha . Lazima tuwe na mtazamo sahihi katika kufikiri na kutoa majibu sahihi. Yanga SC kimbinu na kiufundi ina wachezaji wengi ambao ni averaged players . Wachezaji kiwango cha wastani ambao wanakosa basics nyingi kimbinu na kiufundi na hili si kwa Yanga tu ni sehemu kubwa ya nchi yetu kwa sababu hatuna misingi mizuri huko chini.
Ngoma ameingia katika mechi hii akiwa hayupo sawa kwa zaidi ya asilimia 50 lakini 50 zilizobaki ndizo alizotusaidia kuwatuliza wazambia kule mbele na kuanzisha move ya goli. Jiulize asingecheza kabisa ingekuwaje?!. Kocha kamtoa nje baada ya hali yake kuwa tete na kuanza kucheza kwa woga kwa hofu ya kuumia. Hofu yake ilianza kuwapa amani Zanaco na kucheza free. Kocha kamtoa nje na kumwingiza Emanuel ili kuendeleza tempo ya mchezo lakini Martin kapoteza nafasi nne za wazi kwa kukosa utulivu na umakini kimbinu . Lwandamina aingie kucheza ?
Kamusoko majeruhi wa mechi ya watani wa jadi. Leo kaanza kama kiungo mshambuliaji akiwa bado hajapona sawa . Na imelazimika kupangwa baada ya Tambwe kuwa bado majeruhi na Niyonzima kuchelewa mazoezi . Amefanya mazoezi siku mbili tu akikosekana zaidi ya siku sita ! anatoa wapi match fitness?! Apangwe aitwe muhujumu tena ?! au kuvunja morali ya waliotoka jasho juma zima?! Kumpa nafasi Kamusoko GL alicheza vyema kamari lakini kutoneshwa na kuanza kucheza kwa hofu ilimlazimu kocha kumtoa .
Shida moja ya Mahadhi hajatambua kama GL anamwamini na anatamani afanikiwe. Mabadiliko yake kwa Kamusoko yalilenga vitu viwili ambavyo yeye imekuwa tatizo kuvitimiza. Kwanza ku " mantain " mashambulizi na kuhakikisha mpira mbele unakaa na cha pili kuhakikisha muunganiko wake na viungo chini yake unaimarishwa katika " direct play ". Mahadhi kaingia akawa flat & floppy na kuwaruhusu Zanaco kuwa na mipango mizuri toka chini hali iliyofanya kiungo chote cha Yanga kuvamiwa na kumtoa kabisa mchezoni Zulu kwenye mipango ya kushambulia na kujikuta wakijikusanya kati na Yondani bila mwelekeo.
Jicho la GL likaamua kumtoa Zulu na kumleta Kaseke; kwanza awape back up Mahadhi na Yondani pili ajaribu kuisukuma timu mbele . Kidogo hii ilisaidia.
Bado Yanga ina nafasi ya kushinda ugenini endapo hawa majeruhi watakuwa safi na Haruna kucheza . Lakini timu inahitaji " build up " kubwa kiufundi kwa aidha wachezaji kubadilika na kucheza kama matured players wanaoweza kutafuta goli na kulilinda.
Narudia tena tazameni timu yenu , mahesabu wanayotumia waalimu na uwezo wa mchezaji mmoja mmoja kabla ya kumlaumu mwalimu.
Kwanini Zulu hajatumika kama kiungo mkabaji?
Endapo Kamusoko angekuwa vyema kwa asilimia 100 . Yaani mzuri kwenye battling bila hofu ya kujitonesha ? Ni dhahiri kocha angeanza na Zulu chini , Kamusoko juu , Ngoma tisa na kumi Chirwa na pembeni Kaseke lakini Kamusoko na Ngoma wameingia kama kamari hivyo lazima nyuma yao uwape mtu wa back up . Mtu ambaye anaweza kufuta makosa yao kwenye marking pia kuwafungulia njia ili wacheze soka kwenye open space ndio maana Zulu akapangwa juu kama box to box na chini yake Yondani . Ni kama kocha alipandisha ukuta wa marking kwa juu ya Nadir na Bossou kumweka Yondani na amefanya kazi nzuri kabla ya kiungo chao kuvurugwa kwa mabadiliko.
Mtazamo wangu

USIURUHUSU MOYO WAKO ULIPIZE KISASI NA MWL: CHRISTOPHER MWAKASEGE

Usilipize Kisasi! Unasikia? Hata ikiwa umefanyiwa ubaya wa namna gani, Biblia inafundisha na inakusihi usilipize kisasi kwa huyo aliyekufanyia ubaya. Biblia inasema hivi:
" Wapenzi, msijilipizie kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, kisasi ni juu yangu Mimi, Mimi nitalipa, anena Bwana " (Warumi 12:19)
Kuna hasara zinazoweza kukupata ukiamua kulipa kisasi kwa mambo uliyofanyiwa ambayo hayakupendezi. Ikiwa ni masuala ya kikabila, usilipe kisasi. Ikiwa ni masuala ya kidini, usilipe kisasi. Ikiwa ni masuala ya kifamilia, usilipe kisasi. Ikiwa ni masuala ya kikazi, usilipe kisasi. Ikiwa ni masuala ya uhusiano wako na majirani zako, usilipe kisasi.Ndiyo! Usilipe kisasi! Kwa nini? Kwa sababu " imeandikwa kisasi ni juu yangu Mimi; Mimi nitalipa, anena Bwana ".
Lakini ikiwa utaona ya kuwa Mungu hawezi kukusaidia na ukaamua kujichukulia madaraka ya kujilipiza kisasi hasara zifuatazo hakika zitakupata!
Hasara ya Kwanza "UTASHINDWA!"
Katika jambo lolote lile lililokukasirisha - liwe la kidini, au kikabila, au kifamilia, au kikazi, na kadhalika ukiamua kulipa kisasi utashindwa wewe kwa sababu vita hivyo si vya mwili na wala silaha ambazo Mungu amekupa si za mwili! Tunasema hivi kwa sababu katika  2 Wakorintho 10:3- 5 imeandikwa hivi:" Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi yamwili; maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome, tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikra ipate kumtii Kristo ".
Soma: Tabia 8 Za Watu Wapole - Dr. Chris Mauki.
Tena katika kitabu cha Waefeso 6:12 imeandikwa hivi: " Kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho ".
Uwanja wa mapambano uliyonayo ni " katika ulimwengu wa roho " na mapambano uliyo nayo " si juu ya damu na nyama " - ingawa unaona ya kuwa ni watu na ni binadamu kama wewe wanaokusonga - lakini fahamu hili ya kuwa wanatumiwa tu na ibilisi!
Mbinu mojawapo ya shetani anayotumia akitaka kukuangamiza ni kukufanyia kitu kitakachokukasirisha ili uamue kujibu au kushindana kimwili kwa sababu anajua ukishindana " kimwili " au katika mwili utashindwa hakika, maana vita hivyo si vya mwili wala silaha ambazo Mungu amekupa si za mwili!
Hasara ya Pili "MATATIZO HAYATAKWISHA!"
Kumbuka imeandikwa hivi katika kitabu cha Wagalatia 6:7; " Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa chochote ampandacho mtu. Ndicho atakachovuna ".
Ikiwa umeamua kulipa kisasi kwa kumfanyia ubaya yule aliyekufanyia - ubaya hautakwisha, kwa sababu utavuna ulichopanda.Ndiyo maana imeandikwa hivi:" Yeye arudishaye mabaya badala ya mema, mabaya hayataondoka nyumbani mwake " (Mithali 17:13)
Ukiamua kulipiza kisasi kwa kumfanyia ubaya yule wa nyumbani mwako - Biblia inasema " mabaya hayataondoka nyumbani mwako " Hii ndiyo maana matatizo mengi katika ndoa na katika jamii hayaishi - kwa sababu mtu akifanyiwa ubaya naye analipa kisasi.
Ukiamua kulipa kisasi kwa kumfanyia ubaya yule wa nchini mwako ujue hakika mabaya hayataondoka nchini mwako. Hili ndilo lililowapata wenzetu wa nchi za Burundi na Rwanda - kulipizana kisasi - matokeo ni uhasama usiotaka kupotea - pamoja na juhudi zote za kimataifa kutafuta suluhisho.
Ukiamua kulipa kisasi kwa kumfanyia ubaya yule wa kazini kwako - fahamu mabaya hayataondoka kazini kwako. Ikiwa ni shuleni - mabaya hayataondoka hapo shuleni.
Tena hali ya mwisho inakuwa mbaya zaidi,kila wakati kisasi kinapoendelea kupandwa. Kwa sababu ukiwapa watu ubaya - nawe utapewa ubaya kwa; " kipimo cha kujaa na kushidiliwa, na kusukwa sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile upimacho ndicho mtakachopimiwa" (Luka 6:38)
Soma: Jifunze Kusamehe - Mwalimu Christopher Mwakasege
Kumbuka ubaya haushindwi na ubaya mwingine, bali unashindwa na wema kama vile dawa ya chuki si chuki bali upendo! Ndiyo maana Warumi 12:21 inasema; "Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema ".

Tuesday, March 7, 2017

MAFANIKIO YAKO YAMEJIFICHA HAPA

    MAFANIKIO YAKO YAMEJIFICHA HAPA.
                                 👇👇

√Yapo matokeo ambayo katika maisha yako wewe huwezi kuyaona hapo hapo wala mwingine pia hawezi kuyaona kwako. Kwa mfano, unaposoma kitabu huwezi kuona matokea yake leo au kesho moja kwa moja, inachukua muda fulani.

•Kwa hiyo unaona kama yapo matokeo ambayo huwezi kuyaona moja kwa moja, hapa ndipo unapotakiwa kuwa mwangalifu sana na maamuzi yote yote hasa katika vile unavyovifanya katika maisha yako.

•Utake usitake, maamuzi yoyote yatakupa matunda au matokeo hata kama ni kidogo sana. Hapa sasa ndipo unapotakiwa ujue mafanikio kama mafanikio yanajengwa kwenye mstari mwembamba sana ambao wengi wanashindwa kuutambua.

•Tofauti ya tajiri na maskini ndipo huanza kujitokeza, kwa mfano matajiri hujali sana kupata matokeo yasiyoonekana, tofauti na watu maskini ambao wao hutaka papo kwa papo, hutaka mambo yaonekane tu.

•Kuwa makini sana na mambo unayoyafanya, kila jambo lifanye kwa faida, ili ukianza kuvuna matokeo usiyoyaona miaka kumi ijayo usije ukashikwa na mshangao, kwamba ‘alaa hivi kumbe nilikosea wapi.’

•Ndio maana tunasema hivi hata yale maamuzi unayoyafanya leo, hayana uwezo wa kuathiri maisha yako kesho, kesho kutwa au mwakani, ila matokea ya maamuzi yako unaweza ukaanza kuyaona hata baada ya miaka mitatu, miaka mitano au hata zaidi ya hapo kabisa.

•Kila wakati kuwa makini na maamuzi yako, kuwa na maamuzi ya busara. Kama utakuwa na maamuzi mabovu usishangae ukaja kukuta maisha yako tayari yameshaharibika na itakuwa ngumu sana kwako kuanza upya kurekebisha kwani itachukua muda pia.

•Hakuna wa kukufanya ushindwe au kukuonea kwenye maisha yako. Kila kitu unacho wewe. Tambua kabisa yapo matokeo yasiyoonekana leo kwenye maisha yako, angalia matokeo hayo yasiweze kukupoteza.

•Chunga matumizi yako ya pesa, angalia uhusiano wako na watu wengine, fanya kila unavyoweza kufanya kila kitu kiwe kwa ubora kwako hata kama huna matokeo yasiyoonekana. Matokeo hayo ipo siku yataonekna na yatakuwa nje.

•Sasa usije ukawa miongoni mwa wale watakaolia kwa sababu ya kuvuna matokeo mabovu, ya mambo ambayo hawakutarajia yatakuja kuonekana. Fanya vitu vyenye maana, upate matokeo yanayoonekana mbeleni.

Saturday, February 4, 2017

UMUHIMU WA MAJI MWILINI NI MKUBWA KULIKO UZANIAVYO

'MAJI'

Asilimia 75 ya mwili wa Binadamu ni maji, hivyo kila ogani ndani ya mwili haiwezi kufanya kazi bila ya maji.

Kabla haujawaza Soda, Kahawa, Bia, Divai ama kinywaji kingine chochote waza maji safi na salama kwa kunywa

Unajua maji yanafaida nyingi sana,
• Yanasaidia mmeng'enyo wa chakula (kulainisha chakula) hivyo kupata choo laini • Yanaboresha sana afya ya ngozi •Yanasaidia kinga za mwili •Yanasaidia kupunguza uzito (mafuta) mwilini •Yanasaidia kujenga afya ya figo na Ini (ni kichocheo kizuri cha kuondoa sumu mwilini) • Yanasaidia damu isigande •Yanaongeza oxygen na hivyo kufanya damu kuwa na oxygen ya kutosha na kuweza kufika kila mahali kwa urahisi (upunguza maumivu ya kichwa) •Yanapooza mwili (kuondoa uchovu)
•Yanasaidia mfumo wa upumuaji (mapafu)
Na faida nyinginezo nyingi.

Kunywa maji mara uamkapo
Kunywa maji dakika 30 kabla ya chai
Kunywa maji lisaa limoja baada ya chai
Kunywa maji dakika 30 kabla ya chakula cha mchana
Kunywa maji saa moja baada ya chakula cha mchana
Kunywa maji nusu saa kabla ya chakula cha jioni
Kunywa maji saa moja baada ya chakula
Kunywa maji kabla ya kulala
Kunywa maji kabla ya kusikia kiu.

Tuesday, January 24, 2017

MAARIFA ZAIDI KILA KUKICHA TUNA JARIBU KUKUMBUSHANA

MAARIFA ZAIDI

Maisha ni Mfumo halisi katika ulimwengu halisi

Katika maisha hakuna kuigiza au mazoezi kila jambo unalolifanya lina matokeo yake

Na matokeo haya wengine tunaweza yaita ni matunda

Na matokeo haya ambayo yanaibuka baada ya jambo ulilolifanya au kuliwaza au kuliongea huweza kuwa chanya au hasi

Mara zote hakuna binadamu ambaye yuko tayari katika maisha yake binafsi akutane na matokeo hasi... siku zoooote hupenda apate chanya tu katika maisha yake...

Lakini kati ya wanadamu weeengi ambao wanataka wao wewe na chanya tu katika maisha yao hasa kwa matendo na maamuzi wafanyayo lakini pia hupenda sana hata ndugu na jamaa na marafiki na majirani walete mchango chanya katika maisha yao

Mithali 31:12
[12]Humtendea mema wala si mabaya,
Siku zote za maisha yake.

Ukisoma huu mstari kuna jamno hapo

Lakini pia katika maisha yetu wanadamu tunawaza mengi na kufanya mengi lakini Mungu hutuwazia mema.

Katika Zaburi ya 23:6

Anazungumzia swala la fadhili za Bwana kumfuata siku zooooote za maisha yake.....

Endapo ukifanya yampendezayo Mungu basi tegemea fadhili na baraka za Bwana kuwa juu yako....

Lakini pia sio kwa Mungu tu hata kwa Jirani yako, ndugu, rafiki, na wengineo wote ukitaka wakuwazie mawazo mema na kukutendea yaliyomema jifunze kutenda mema kila siku kwao na ukiwakosea jifunze kuomba radhi

Jambo usilopenda kutendewa hakikisha humtendei jirani yako....

Kutoka 20:16
[16]Usimshuhudie jirani yako uongo.

Zaburi 101:5
[5]Amsingiziaye jirani yake kwa siri,
Huyo nitamharibu.
Mwenye macho ya kiburi na moyo wa majivuno,
Huyo sitavumilia naye.

Mithali 11:9
[9]Asiyemcha Mungu humpoteza jirani yake kwa kinywa chake;
Bali wenye haki watapona kwa maarifa.

Marko 12:31
[31]Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.

Warumi 15:2
[2]Kila mtu miongoni mwetu na ampendeze jirani yake, apate wema, akajengwe.

Hii ni baadhi tu ya Mistari kwenye Biblia inayoonyesha ni vyema kutenda mema kwa Jirani yako

Na hii itakusaidia kustawi katika maisha yako maana hataacha kukuwazia mema na kukufanya kupata mrejesho chanya toka kwa kwao.....

Mwisho: Hakuna ambaye anapenda kuwa na rafiki au jirani asiyefanana na malengo yake au kuendana na mfumo wake wa maisha. Lakini tambua kila mtu anakusudi katika Maisha yako ya kila siku. Usimdharau yeyote kwa umri, kipato, jinsia, au namna yoyote ile... Biblia inasema Hata wabaya waliumbwa kwa wakati wa ubaya.... Upendo ndio silaha yetu....

Upendo Huvumilia, Hauhesabu mabaya.........

Wakolosai 3:14
[14]Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.

2017--Maarifa Akilini, Speed Unyayoni

THINK AND GLOW RICH Inspirational and Motivational Inc

Monday, January 23, 2017

SAFARI YA COMORO:

SAFARI YA COMORO:
Ndugu wana Yanga kama mnavyofahamu timu yetu ipo  ktk maandalizi ya mechi za Club Bingwa Africa. Mechi yetu ya kwanza tunaanzia Moroni Comoro tarehe 12/2/2017.
Wale wanaohitaji kwenda kuisupport timu yetu pendwa taratibu za usafiri ni kama ifuatavyo:
1. Ndege  ya bei  nafuu ni ATCL karibia USD 430 kwenda na kurudi ingawa inaweza kupungua  tukienda kama group. Dirisha la nauli kwa mwezi Feb inataraji kufunguliwa leo au kesho tutawajulisha nauli halisi.
2. ATCLl inafanya safari zake huko siku  3 kwa wiki J4, Alhamis na Jumamosi. Hivyo   tarehe nzuri ya mashabiki kusafiri ni 11/2/2017 na kurudi 14/2/2017
3. Visa ni 'on arrival' uenda malipo ya visa yasizidi USD 50 au chini ya hapo
4. Kwa waliokusudia kusafiri ni sharti uwe  na Passport ya kitabu iwe haita kwisha muda wake kabla ya tarehe 14/2/2017
Pia cheti  cha kinga ya homa ya manjano(yellow fever)
5. Wale wote walio tayari mnaombwa kujiorodhesha hapa au club ili iwe rahisi kufanyiwa wepesi wa safari yetu kwa kuhusisha uongozi wa club, tunafanya mawasiliano na Katibu wetu wa Yanga juu ya safari hii.
SHIME WANA YANGA MSIMU WETU NDIO HUU. TUONYESHE MSHIKAMANO WETU TWENDENI KWA WINGI TUWAPIGIE HUKOHUKO KWAO.
DAIMA MBELE

MECHI YA SIMBA NA YANGA YASOGEZWA MBELE

MECHI YA SIMBA NA YANGA YASOGEZWA MBELE

BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE / 17 minutes ago

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MCHEZO wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baina ya mahasimu, Simba na Yanga umesogezwa mbele hadi Februari 25, kutoka Februari 18, mwaka huu.
Habari kutoka ndani ya Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema kwamba sababu ya kusogezwa mbele kwa mchezo huo ni muingiliano na Ratiba ya michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika.

Februari 10, mwaka huu, Yanga watakuwa wageni wa Ngaya FC katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Mde mjini Mde nchini Comoro, kabla ya kurudiana Februari 17, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa sababu hiyo, mchezo wa Simba na Yanga usingeweza kufanyika tena Februari 18 na busara za TFF zimeupeleka hadi Februari 25.

KITUO CHA MWENDO KASI CHA POSTA NI GENGE LA VIBAKA

KITUO CHA MWENDO KASI CHA POSTA NI GENGE LA VIBAKA.

Nilikuwa natoka shule mnazi mmoja kama saa sita kasoro jana jumapili tar 22/01/2017, kwa mwendo kasi nikashuka kituo cha posta cha mwendo kasi, ili niingie kazini kujisomea, sasa ninavyotembea pembeni ya ukuta wa Luther House, dereva wa guta barabarani akiwa ananipita akanisalimia halafu akaniambia, geuka nyuma kuna vijana wawili nyuma yako sio wazuri jiangalie sana. Sasa mimi nilivyotizama nikaona mmoja ana rasta na mwingine wa kawaida ni wa kawaida sana na ninawamudu lakini nyuma yao nikaona kama kuna kundi hivi. Wote wako umbali kama wa mita hamsini, nikaamua kutembea haraka hatua chache halafu nikavuka barabara ili niwapoteze, nao kwa wakavuka barabara pia ndipo nikavuka kurudi usawa nilipokuwa awali maana nilikuwa nimeshafika getini.

Wakati ninamsimulia mlinzi akaja kijana mmoja yuko na mountain bike anasema yeye ni msamaria mwema, akanieleza nina bahati sana lile kundi lote lilikuwa linakuja kwa ajili yangu. Nikajiuliza hivi amejuaje wakati mimi mwenyewe nimefanya kushtuliwa. Ndio hapo akasema vibaka wanadhani ndani ya hilo begi kuna laptop au video cameras na hivi una kitambi nimewachanganya. Nikamwambia hao wezi ni wapuuzi sana huku nikimfungulia begi nikamwambia nimetoka shule nakuja kujisomea kazini, nilichojaza humu ni madaftari tu. Akaangalia kwa kushtuka sana kana kwamba naye alikuwa na shauku ya kuona kilichomo. Nikamtilia mashaka bila kusema ila nilimkariri mavazi. Nikaingia ofisini nikasoma hadi saa kumi na moja ila wakati natoka walinzi wakanishauri niliache lile begi, nami nikatoka bila begi. Ninavyotoka nje ya geti sikuona mtu yeyote ninayemkumbuka wala kumjua ila wakati nimebakiza mita hamsini kufika kituo cha mwendo kasi hicho cha posta, hamad!! nikamwona yule msamaria mwema na mountain bike yake akiwa upande wa pili wa barabara akiendesha taratibu kana kwamba ananisindikizia mithili ya wale walinzi wa kisirisiri (Secret Service)

Nilichojifunza ndugu zangu ni hiki kifuatacho.
1. Usitembee njia yenye watu wachache hasa wakati wa weekend tena ukiwa na fedha nyingi au vitu vya kuvutia kama mabegi haya ya laptop, mabegi ya mgongoni hizi backpacks, simu na tablets.
2. Usipende kusimama kusaidia watu wanaotaka msaada kwako maana hao ni wapelelezi wa wezi kazi yao ni kutoa ishara tu uvamiwe.
3. Kuwa makini na watu walio pembeni yako na nyuma yako na kama kuna uwezekano weka umbali wa kutosha kama ni njia yenye watu wachache sana.
4. Acha mazoea ya kutembea usiku utakuwa wewe ndio umewaingilia wezi kwenye kazi yao.

Ukweli ni kuwa siku za weekend kuna vibaka katika njia zenye watu wachache. Kuweni makini sana sa hivi watu hawana hela vijana waliokata tamaa wameamua kuitafuta kwa nguvu, na wamejipanga vizuri wana roles na responsibilities hadi za ku-act kama decoy, wanajifanya wasamaria kumbe ndo wanakuangamiza.

Thursday, January 19, 2017

HAMORROIDS AU BAWASIRI

HAMORROIDS AU BAWASIRI
Bawasiri ni mojawapo ya tatizo ambalo mara nyingi linapotokea humfanya mtu kuwa na aibu kuelezea au kwenda hospitali ili kupata tiba sahihi. Bawasiri au hemorrhoids husababishwa na kuvimba kwa mishipa ya damu aina ya vena katika eneo la mfereji wa haja kubwa.
 
AINA ZA BAWASIRI
NJE
Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huweza kuambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina kitaalamu inaitwa Thrombosed hemorrhoid.NDANI 
Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu na wengi huwa hawatambui kuwa wanatatizo hili. 
Aina hii imegawanyika katika mainisho yafuatayo:Daraja I- Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
Daraja II- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja III- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja IV- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.
Je bawasiri husababishwa na nini?

BAWASIRI HUSABABISHWA NA NINI?
Bawasiri husababishwa na;
Tatizo sugu la kuharishaKupata kinyesi kigumuUjauzitoUzito kupita kiasi (obesity)Kupenda kufanya ngono ya njia ya haja kubwa (anal sex)Kwa ujumla mambo yanayo ongeza shiniko katika tumbo.Umri mkubwaDALILI ZA BAWASIRI 
Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia (hematochezia)Maumivu au usumbufuKinyesi kuvujaKijiuvimbe katika eneo la tundu la haja kubwaNgozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwaKujitokeza kwa kinyama (bawasiri) wakati wa haja kubwa
MATATIZO YANAYOWEZA KUTOKEA KUTOKANA NA BAWASIRI
Upungufu wa damu mwilini (Anemia)Strangulated hemorrhoids
VIPIMO NA UCHUNGUZI
Digital rectal examinationKipimo cha njia ya haja kubwa (Proctoscope)Kipimo cha utumbo mpana (Sigmoidoscope)
MATIBABU
Matibabu hutegemea na hali na aina ya Bawasiri
Rubber band ligation - Hapa mishipa hufungwa na rubber band ili kuzuia damu kwenda kwenye eneo liloathirika, na hutumika kwenye aina ya ndani ya bawasiri.Sclerotherapy- Hapa kemikali huwekwa kwa njia ya sindanoCoagulation (infrared, laser and bipolar)Upasuaji;         Hemorrhoidectomy 
         Stapled hemorrhoidopexy

 
NJIA ZA KUZUIA BAWASIRI 
High fibre diet, kula mboga za majani, matunda, na nafaka kwa wingi.Kunywa maji mengi kwa siku (glasi sita had nane kwa siku)Punguza kukaa kwa muda mrefu sana hasa ukiwa chooni, kwa sababu unaweza kuongeza shinikizo katika mfereji wa haja kubwa 
DAWA YA MARADHI YA BAWASIRI ZA AINA ZOTE
 
Ndugu zangu kichwa hapo juu chaweza kumfanya mtu ajiulize swali, je bawasiri zipo za aina ngapi?
Jawabu ni kuwa bawasiri zipo za aina mbili. 
Aina inayotembea (Yaani ikitoka ndani na kurudi) Aina inayosimama (Yaani kinyama kinachoota kwenye dubuni).Sasa bawasiri zote hizi tiba yake n hizi zifuatazo

Kitunguu swaumu (Vijiko vitatu vya chakula)Asali (Nusu lita)Tangawizi (Vijiko vitatu vya chakula)Mbegu za Figili (CELERY) - (Vijiko vitatu vya chakula)Matumizi: Madawa haya lazima yapimwe kwa idadi hiyo yakiwa tayari yamekuwa unga, kisha changanya pamoja, na dozi yake ni kama ifuatayo;Kijiko kimoja cha unga wa madawa haya utakilamba asubuhi, mchana utafanya kama hivyo tena kisha jioni yaani (1 X 3) kwa muda wa siku saba hadi kumi na moja (7 - 11).

Tuesday, January 17, 2017

NI KKKT -KIMARA TENAA SI YA KUKOSA

YAH: TAMASHA/IBADA YA KUSIFU NA KUABUDU UMOJA WA VIJANA DAYOSISI

Wapendwa VIJANA ninawasalimu BWANA WETU YESU KRISTO ASIFIWE.

Ninawajulisha kuwa Kwa mujibu wa KALENDA YA MATUKIO YA VIJANA 2017 kutakuwa na TAMASHA/IBADA YA KUSIFU NA KUABUDU NGAZI YA DAYOSISI.

Mahali: USHARIKA WA KIMARA uliopo Jimbo la Magharibi.

Tarehe: 22/01/2017.

Siku: Jumapili hii

Muda: Kuanzia Saa 7:00 Mchana.

WAHUSIKA: VIJANA WOTE KUTOKA MAJIMBO YOTE NA SHARIKA NA MITAA YOTE ndani ya DMP.

**********************

Njooni wote TUSIFU, TUABUDU, TUOMBE KWA PAMOJA NA TUMKABIDHI MUNGU MIPANGO YETU VIJANA KWA MWAKA 2017.

*****-***************

Ninawakaribisha sana katika tukio hilo, na ninawatakia Maandalizi mema na MUNGU wa MBINGUNI awe nanyi katika maandalizi na usikose kuombea tukio hilo.

Kwa maana mmeokolewa kwa neema...........Waefeso 2:8

************-*--*---**

ANANIA NDONDOLE

M/Kiti
Umoja wa Vijana Dayosisi

MAARIFA ZAIDI

                         MAARIFA ZAIDI

Ni kweli Mwaka jana 2016 hukufanikisha jambo la kiuwekezaji japo hukuwahi kulala njaa..

Hii inamaana kuwa mipango yako yote uliwekeza katika kuishi na si kuishi katika kufikia malengo makubwa kwaajili ya siku za usoni.

Zingatia machache haya:

1. Usikubali kuishi kwa kutegemea chanzo kimoja cha mapato

2. Usiweke akiba baada ya kufanya matumizi weka akiba kabla ya matumizi

3. Mtafute Muumba wako kwa nguvu zako zote na akili zako zote

4. Fikiri kabla ya kutenda jambo..

2017- Maarifa akilini, Speed Unyayoni

                 Be blessed .....!!!!!

SEMINA YA MWAKASEGE JIJINI ARUSHA

🌂2⃣ SEMINA YA NENO LA MUNGU ARUSHA UWANJA WA RELI

TUMIA AKILI KIROHO ILI UFANIKIWE KIMAISHA

NA MWL CHRISTPHER MWAKASEGE

16-JANUARY -2017

Bwana Yesu asifiwe Napenda kuwakaribisha wenzetu waliojiunga nasi leo kwa mara ya Kwanza redio uzima kutoka Dodoma inayopatikana maeneo ya Dodoma, Babati Iringa na Singida. Na redio zinazorusha semina hii angalia pale mwisho utaziona zote na frequency zake. Na tuambie unatupata toka wapi kwa kutuma msg katika namba hizi
+255715511633
+255682657050
+255767511633

RADIO ZINAZORUSHA
SEMINA LIVE ARUSHA.
15 – 22 JANUARY, 2017
6 KUANZIA SAA KUMI HADI SAA 12 JIONI

#FREQUENCY & #COVERAGE
1. SAFINA – ARUSHA
Arusha – 92.5 Mhz
Tanga – 93.4 Mhz
Singida – 106.1 Mhz
Kigoma – 106.1 Mhz
Iringa – 105.7 Mhz
Arusha, Tanga (Lushoto), Singida, Kigoma na Iringa.

2. SAUTI YA INJILI – MOSHI
Arusha – 96.1
Moshi – 92.2
Same – 100.4
Rombo – 96.4
Tanga – 102.6
Mlalo Tanga – 96.7
Manyara – 102.9
Morogoro – 99.9
96.1 – Arusha, babati, karatu, mtowambu, musoma vijijini.
96.4 – Taveta, Rongai, Voi
102.6 – Unguja na Pemba, Mombasa
102.9 – Dodoma ( Kondoa, Chemba, Chamwino, Kibaigwa)
99.9 – Kiluvya, Rufiji, Pwani, Tegeta, Ubungo, Manzese, Mbezi, Ruaha, Lindi (Daraja la Mkapa).
www.sautiyainjili.org

3. HHC ALIVE FM – MWANZA.
91.9 FM
Mwanza, Simiyu, Mara, Shinyanga, Geita na Kagera.

4. RUNGWE FM – TUKUYU.
102.5 FM
Kyela, Ileje, Makete/Njombe, Mbozi – Sumbawanga, Malawi na Mbeya.

5. UPENDO – DAR ES SALAAM.
107.7 FM

-Dar es salaam, Morogoro (Siyo yote)
Zanzibar (baadhi ya maeneo), Tanga (baadhi ya maeneo), Pwani.

6. BARAKA – MBEYA.
107.6 FM
Mbeya, Njombe (Siyo yote), Songwe (Kidogo), Rukwa – kidogo, Iringa baadhi ya maeneo (Mafinga).

7. INFO – MTWARA.
92.1 FM
Mtwara, Lindi ( Maeneo ya vijijini haisikiki vizuri).

8. STARTER – NJOMBE.
90.7 FM
- Njombe , Iringa (Mufindi), Mbeya (Mbarali), Tunduma

*9. *REDIO CG FM*
*89.5FM*

- Tabora, Kigoma, Katavi, Singida

10 REDIO UZIMA YA DODOMA

-Dodoma,Babati,Iringa na Singida

MAMBO 3 YA LEO

1 Akili ni eneo ndani ya nafsi ya mtu lililoumbwa kwa mfano wa Mungu
_Mithali 3:19 Kwa hekima Bwana aliiweka misingi ya nchi; Kwa akili zake akazifanya mbingu imara _kwa hiyo Mungu anakili.  Sasa unganisha na _1 Yohana 5:20 Nasi twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele._

>>Kwa hiyo Mungu alipokuwa anamuumba mtu alimpa na akili maana katika akili ndipo tunakuwa mfano wa Mungu. Ukisoma kitabu cha Mwanzo utaona jinsi Mungu aliumba roho ya Mtu kwanza na baadae akampa mwili kutoka kwenye udongo na mwishoni ndipoalipo mpulinzia pumzi na akawa nafsi hai.
>>Ndani ya nafsi kuna akili, na lakini ubongo upo kwenye mwili.  Ila kumbuka kuna uhusiano kati ya ubongo  na tutazama huko mbele.

2 Mungu anataka tujifunze nini kwa kutujulisha kuwa alitumia akili ili kuumba mbingu
_Mithali 3:19-20 Kwa hekima Bwana aliiweka misingi ya nchi; Kwa akili zake akazifanya mbingu imara; Kwa maarifa yake vilindi viligawanyika; Na mawingu yadondoza umande._
>>Sasa kwanini isitoshe tu kutuambia kuwa Mungu aliumba mbingu na nchi sasa kwanini biblia inaenda ndani kutueleza kuwa wakati mbingu inaumbwa Mungu alitumia kitu gani? Angali tena hiyo mistari.

>>Sasa kwanini Mungu anatupeleka jikoni, unajua ukienda hotelini unahitaji kujua tu kuwa chakula kimeiva na kianenda na ile thamani ya hela uliyolipa. Sasa anapokuja mpishi na kukueleza kuwa kwa kitunguu nilikaangiza mboga, au anaanza kukuambia namna chakula kilivyoandaliwa na namna vitu alikopata na vinavyoandaliwa, unaweza sema haina haja ya mimi kujua ila nataka kujua tu chakula kama kimeiva na kinaendana na ile hela niliyolipa.

>>Kumbuka hili, thamani ya chakula haipo kwenye chakula, ipo kwenye maandalizi ya chakula. Na ndio maana utaona hata cocacola hawatoi siri namna wanavyoanadaa cocacola maana wakikuambia hiyo furmula ina maana siku nyingine na wewe utatengeneza yaa kwako.  Kwa hiyo ndio maana wanabaki nayo wenyewe.

>>Sasa Mungu akikupa akili anataka uende jikoni ili ujue namna ya kuandaa hicho chakula. Angalia mistari ifuatayo
_Ayubu 38: 33 Je! Unazijua *amri zilizoamuriwa mbingu?* Waweza kuyathibitisha mamlaka yake juu ya dunia?_    >>Sasa ukiangalia ile mithali tunajua kuwa Mungu alitumia akili ili kuzifanya mbingu imara, na ile kusema  amri maana yake siyo sheria sasa katika Kiswahili tungesema kanuni yaani order au ordinance.  Maana yake zimewekwa kwa utaratibu na zimetengenezwa kwa mtazamo wa kiutekelezaji.

_Mathayo 5:34 lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu;_  sasa twende pole pole

_Hosea 2: 21-22 Tena itakuwa siku hiyo, mimi nitaitika, asema Bwana; nitaziitikia mbingu, nazo zitaiitikia nchi; nayo nchi itaiitikia nafaka na divai na mafuta; nayo yataiitikia Yezreeli. 

>>Sasa ukisoma kitabu cha Mwanzo 1:1 utaona biblia ikisema hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi, na haisemi nchi na mbingu fuata mtiririko kama biblia inavyosema,  kwa maana nataka kukupeleka jikoni kidogo  na mbingu anazozisema hapa sio hizi maana hizi biblia inazzita anga,  hapa nataka tuone mbingu ambazo ni kiti cha enzi cha Mungu  ambazo zina mamlaka juu ya nchi.

>>Hapo Mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi,  na anataka tuone namna akili ilivyokuwa ikifanya kazi katika uumbaji, si unakumbuka ile _Mithali 3:19 Kwa hekima Bwana aliiweka misingi ya nchi; Kwa akili zake akazifanya mbingu imara;_

Akili imegawanyika katika vitu vikubwa 3

1 Kutengeneza nia ya maisha
2 Kuetengeneza viwango vya maisha
3 Kutengeneza vipaumbele vya maisha

Zote hizi ziko hivyo kwa kufauatana na taratibu za amri.

Watu waliokoka wanapata shida sana wanaposoma maandiko na kuona walichokiona kwenye maandiko na namna maisha yao yalivyo wanapata shida sana, na kwa kuona wako kiroho tu wanajua kila kitu wanatapata hivyo hivyo ,hapana haiku hivyo, akili inatakiwa ifanye kazi au itumike katika vipaumbele vya maisha na vya KiMungu. _Mathayo 6:33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa._ na hawajui maana yake nini huu mstari maana wanakata kuelewa tu kiroho lakini Luka 24:45 ina kataaa maana inataka kwanza wafunuliwe akili zao ili waweze kuelewa maandiko.  Maana ili uelewe vizuri inabidi akili ishiriki.

*3 Akili zinafanya kazi kwa kutumia fikra ili ziweze kufanya majukumu yafuatayo*

~Uhusiano wa ubongo na akili ni kuwa ubongo unasimia maeneo mengi sana kufanya kazi, kwa hiyo kushindwa kwa ubongo kufanya kazi ya kusimamia eneo husika lile eneo nalo linaanza kupata shida.

~Kwa hiyo maeneo hayo yapo ndani ya akili kwa vipengele Fulani.

*a). Kuusaidia kuelewa mambo Kimungu*
_Luka 24:44-49 Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi. *Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko*. Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu. Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya. Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu._

>>Ilitakiwawapewe kwanza ufunuo wa Mungu.  Sasa kwa mfano Mtu akikuuliza ufunuo wa Mungu ana maana gani?

*b). Kukusaidia kupata ufahamu, kwenye Kingereza wameita understanding*

>>Maana yake unapata ufahamu wa neno na mazingira ya Kimungu., kwa hiyo ufahamu unakuwa juu yako ya maisha unayoishi, na mazingira na uhusiano na neno la Mungu. Kwahiyo ukielewa mambo haya hutaweza tena kucopy maisha ya mtu kwa sababu utakuwa unaishi maisha yako original. Kama unafikiri natania kawaulize polisi na watakueleza kuwa finger prints zako hazifanani na za mtu yeyote hapa duniani maana uko wewe mwenyewe.

>>Tulienda mkoa mmoja, na kulikuwa na hoteli nzuri sana  na tuliona hawauzi pombe yaani hamna pombe. Tulikuwa na hamu sana ya kutaka kujua huyu ni mtu wa aina gani aliyekubali  kufanya biashara ya hiteli bila ya kuweka pombe. Na walituambia huyo mtu sio mkristo ni wa dini nyingine, na tulipomfuatilia tuligundua kuwa yeye anakunywa pombe na hanywei hoteli kwake bali sehemu nyingine. Sasa huyu katengeneza aina ya maisha ambayo na yeye mwenyewe hayaishi.

*c). Kupanga matumizi ya kipato na rasilimali ulizonazo kwa kuzingatia vipaumbele vya*
     >>> Muda wa sasa na  baadae.
     >>> Mahitaji yako.
     >>> Mazingira.

_Mwanzo 41:32-33 Na ndoto ya Farao kwa vile ilivyokuja mara mbili, ni kwa sababu neno hilo Mungu amelithibitisha, na Mungu atalitimiza upesi. Basi, *Farao na ajitafutie mtu wa akili na hekima amweke juu ya nchi ya Misri*._

>>Sasa hapa Mungu alimsaidia Yusufu kuandaa mpango wa miaka 14  mfufulizo yaani kipindi cha uwingi na kipindi cha ukame.  Na maandko yanasema Yusufu alisema tafuta mtu mwenye akili na sio mtu wa kiroho. Mungu anatoa taarifa kupitia kwa Yusufu  na kuweza kupangilia  mahitaji kwa akili na hekima.

>>Na nataka uone namna akili ilivyofanya kazi.  _Mwanzo 41:37-38 Neno hilo likawa jema machoni pa Farao, na machoni pa watumwa wake wote. Farao akawaambia watumwa wake, Tupate wapi mtu kama huyu, mwenye roho ya Mungu ndani yake?_

>>Farao alijua anaweza akapata mtu mwenye akili na roho ya Mungu isikae ndani yake, bali lipata mtu wa akili na Roho ya Mungu iko ndani yake.  Kwahiyo jua kuwa Roho Mtakatifu ni mafuta na huwezi kujivunia kuwa umejazwa Roho Mtakatifu na hauna akili ina maana ni sawa sawa na kujivunia  mafuta bila ya kuwa na gari na pia gari bila mafuta halina kazi.

*d). Kukusaidia kupambanua mema na mabaya*

_Waebrania 5:14 Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima, *ambao akili zao*, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya._ *na akili kwa kuzitumia ndipo zinazoea* _2 Wakorintho 4:3-4 Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu._

>>Biblia inasema kuwa Mungu wa dunia hii anapofusha fikra za watu ili isiwazukie Nuru ya injili.  Akili ni Zaidi ya mawazo na kwa sababu hiyo akili zinaona.  Kazi ya akili ni kupambanua mema na mabaya.  Na Mungu aliwapo  waumba Adamu na Hawa alipowawekea mti wa mema na mabaya alikuwa wanatakiwa wajue kupambanua mema na mabaya lakini wao yaliyo mema wakaiona ni mabaya na mabaya wakona ni mema yaani walipata confusion. Biblia inasema katika _Mithali 23:7 a., maana aonanvyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo, au katika tafsiri zingine zinasema afikirivyo, au zingine zinasema awazavyo au atafakarivyo_

>>Shetani akipofusha fikra zako unakuwa na tabu sana maana Mungu anakumbia pita hapa unasema hapa unapita alipokukataza.  Mtu anayetegema akili siku zote ni *Hakubali kushindwa hata siku moja kwa sababu atafsiri kwa kutegemea akili peke yake* na *Hajui maana ya unyeyekevu ili kuoambanua mema na mabaya kwa msaada wa Roho Mtakatifu*.

>>Hapa utaelewa kwanini Mungu aliwapeleka wapelelezi 12 katika nchi ya Kanini kwa siku 40, siku zijazo ntakueleza ni kwanini siku 40  na waliporudi walitofautiana katika kutoa majibu. Ila wawili tu maana hawa ndio walikubali kumuweka Mungu katikati ya Fikra zao kuwa hata kama kuna majitu lazima hayawezi zuia ahadi za Mungu.

>>Nataka nikuulize swali jioni ya leo kuwa *Je unapopambanua maisha yako kujua mema na mabaya, na je akili zako zimelishwa kitu gani ili kujua namna ya kupambanua mema na mabaya?*

>>Wana wa Israel walikosea kupambanua na kujua vipaumbele vya Mungu na ndio maana wengine walikwama na hawakufika katika nchi ya ahadi. Ndio maana nauliza ni kitu gani unatumia kupambanua _Wakorintho 13:11-12 Nilipokuwa mtoto mchanga, nalisema kama mtoto mchanga, nalifahamu kama mtoto mchanga, nalifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto. Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana._

>>Sasa  kama hujabatilisha mambo ya kitoto inakuwa ngumu sana kwako kupambanua mambo vizuri,  maana kuwa wengine wanasema mimi ni wa Paulo na wengine wanasema mimi ni wa Apolo, biblia inasema wote hawa Fikra zao ni za Kitoto.  Kwa sababu wanapambanua maisha kidini  na dini kwao ndiyo kipaumbele.

>>Kwenye akili zako umepeleka kitu gani, je unapambanua mambo kisiasa, au kidini au kiumri au kwa kutumia neno la Mungu. *Unatumia nini kupambanua?*

>>Nilikuwa mkoa mmoja na kiongozi Fulani alinitambulisja kwao kuwa huyu ni Fulani Fulani, wakasema oooh, sawa huyu ndiye anayehubiri ila wakasema hapa haiwezekani maana Umri wako na Mambo unayoyasema ni tofauti sana.  Kwa sababu unajua mambo mengi sana na inaonesha umeishi maisha marefu sana hapa duniani.  Ila hao watu walipambanua kiumri. Ndio maana nakuuliza wewe unapambanua kwa kutumia nini?

>>Ndani yako je unaishi maisha ambayo ndiyo Mungu kakupangia, au umeshindwa kutumia akili na umeamua kuweka pembeni, leo nakumbia katika jina la Yesu rudi kwa Bwana  omba Mungu akusaidie namna ya kuoambanua maisha.

>>Huwa nikienda Israel nikipita katika bustani ile ya getsamane nakumbuka jinsi Yesua laivyokuwa anapambana na mwili wake na aina ya maisha ambayo Mungu aliyakusudia. Na akaanza kwa kusema mawazo yake baba  ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke. Lakini haikuwa mapenzi ya Mungu kikombe kimuepuke, na ahsante Yesu aliomba hadi Mwisho na alivuka. Chukia asingevuka wokovu tungeupata wapi. Hata mimi nikipita pale lazima nifanye toba kwa Mungu kuomba kama kunasehemu nimejiinua Mungu anisaidie au kuna sehemu nakwama Mungu anisaide. Sijajua kwa Upande wako umekwama wapi? Je nawewe umefika mahali unasema kikombe kikuepuke? Jion ya Leo nguvu za Mungu zimetufunika.. Mwambie Mungu akusaidie wapi kwenye akili zako.

>>Baada ya hapo yalifanyika maombi mazito san asana. Ukipata nafasi tembelea Youtube na utapata semina ya leo kwa kungalia link nilizoziweka hapo chini.

SEMINA IKO LIVE  KWA KUTUMIA NJIA ZIFUATAZO ZA INTERNET  KUANZIA SAA 9-12 JION

YouTube
https://www.youtube.com/channel/UC4p4lrpgpNd-9bHPgHJ4xWw

Ustream

http://www.ustream.tv/channel/mwakasegemanaministry

*Internet  radio*
www.mwakasege.org
www.kicheko.com

MAFUNDISHO ZAIDI.

FACEBOOK

https://www.facebook.com/Christopher-Diana-MwakasegeMana-Ministry-132462780111984/

Tovuti.
www.mwakasege.org

Summary za masomo haya na ya nyuma

http://www.gospelkitaa.co.tz/?m=1

http://www.kanisaforum.com/forums/Mafundisho-ya-Biblia/

VIPINDI VYA REDIO KILA WIKI
REDIO SAUTI YA INJILI MOSHI
Kila siku ya jumamosi na jumapili kuanzia saa tatu kamili usiku hadi saa nne usiku.

REDIO UPENDO YA DAR ES SALAAM.
Kila siku ya jumamosi na jumapili kuanzia saa tatu kamili usiku hadi saa nne usiku.

REDIO WAPO YA DAR ES SALAAM.
Kila siku ya Jumatano kuanzia saa tatu kamili usiku hadi saa nne usiku.

REDIO FARAJA YA IRINGA.
Kila siku ya jumamosi na jumapili kuanzia saa tatu kamili usiku hadi saa nne usiku.

REDIO FARAJA YA. SHINYANGA.
Kila siku ya jumamosi na jumapili kuanzia saa tatu kamili usiku hadi saa nne usiku.

REDIO UZIMA DODOMA
Kila siku ya jumamosi na jumapili kuanzia saa tatu kamili usiku hadi saa nne usiku.

REDIO VOICE OF TABORA (V.O.T)
Kila siku ya Jumatano kuanzia saa tatu kamili usiku hadi saa nne usiku.

KUNUA KANDA ZA SEMINA HII NA ZINGINE
http://www.mwakasege.org/nunua.htm na http://www.mwakasege.org/mawasiliano.htm

Ubarikiwe sana na Bwana Yesu.

🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏
*Felix Hezron Mbwanji*
*felixmbwanji@gmail.com*
*+255716918848*(whatsapp)
niandikie kwa maoni na ushauri na maboresho.

Happy birthday Anna Mwaipopo

Happy birthday Anna Mwaipopo
Many wishes for your future s
Also God Be with you mom