Tuesday, January 17, 2017

SEMINA YA MWAKASEGE JIJINI ARUSHA

🌂2⃣ SEMINA YA NENO LA MUNGU ARUSHA UWANJA WA RELI

TUMIA AKILI KIROHO ILI UFANIKIWE KIMAISHA

NA MWL CHRISTPHER MWAKASEGE

16-JANUARY -2017

Bwana Yesu asifiwe Napenda kuwakaribisha wenzetu waliojiunga nasi leo kwa mara ya Kwanza redio uzima kutoka Dodoma inayopatikana maeneo ya Dodoma, Babati Iringa na Singida. Na redio zinazorusha semina hii angalia pale mwisho utaziona zote na frequency zake. Na tuambie unatupata toka wapi kwa kutuma msg katika namba hizi
+255715511633
+255682657050
+255767511633

RADIO ZINAZORUSHA
SEMINA LIVE ARUSHA.
15 – 22 JANUARY, 2017
6 KUANZIA SAA KUMI HADI SAA 12 JIONI

#FREQUENCY & #COVERAGE
1. SAFINA – ARUSHA
Arusha – 92.5 Mhz
Tanga – 93.4 Mhz
Singida – 106.1 Mhz
Kigoma – 106.1 Mhz
Iringa – 105.7 Mhz
Arusha, Tanga (Lushoto), Singida, Kigoma na Iringa.

2. SAUTI YA INJILI – MOSHI
Arusha – 96.1
Moshi – 92.2
Same – 100.4
Rombo – 96.4
Tanga – 102.6
Mlalo Tanga – 96.7
Manyara – 102.9
Morogoro – 99.9
96.1 – Arusha, babati, karatu, mtowambu, musoma vijijini.
96.4 – Taveta, Rongai, Voi
102.6 – Unguja na Pemba, Mombasa
102.9 – Dodoma ( Kondoa, Chemba, Chamwino, Kibaigwa)
99.9 – Kiluvya, Rufiji, Pwani, Tegeta, Ubungo, Manzese, Mbezi, Ruaha, Lindi (Daraja la Mkapa).
www.sautiyainjili.org

3. HHC ALIVE FM – MWANZA.
91.9 FM
Mwanza, Simiyu, Mara, Shinyanga, Geita na Kagera.

4. RUNGWE FM – TUKUYU.
102.5 FM
Kyela, Ileje, Makete/Njombe, Mbozi – Sumbawanga, Malawi na Mbeya.

5. UPENDO – DAR ES SALAAM.
107.7 FM

-Dar es salaam, Morogoro (Siyo yote)
Zanzibar (baadhi ya maeneo), Tanga (baadhi ya maeneo), Pwani.

6. BARAKA – MBEYA.
107.6 FM
Mbeya, Njombe (Siyo yote), Songwe (Kidogo), Rukwa – kidogo, Iringa baadhi ya maeneo (Mafinga).

7. INFO – MTWARA.
92.1 FM
Mtwara, Lindi ( Maeneo ya vijijini haisikiki vizuri).

8. STARTER – NJOMBE.
90.7 FM
- Njombe , Iringa (Mufindi), Mbeya (Mbarali), Tunduma

*9. *REDIO CG FM*
*89.5FM*

- Tabora, Kigoma, Katavi, Singida

10 REDIO UZIMA YA DODOMA

-Dodoma,Babati,Iringa na Singida

MAMBO 3 YA LEO

1 Akili ni eneo ndani ya nafsi ya mtu lililoumbwa kwa mfano wa Mungu
_Mithali 3:19 Kwa hekima Bwana aliiweka misingi ya nchi; Kwa akili zake akazifanya mbingu imara _kwa hiyo Mungu anakili.  Sasa unganisha na _1 Yohana 5:20 Nasi twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele._

>>Kwa hiyo Mungu alipokuwa anamuumba mtu alimpa na akili maana katika akili ndipo tunakuwa mfano wa Mungu. Ukisoma kitabu cha Mwanzo utaona jinsi Mungu aliumba roho ya Mtu kwanza na baadae akampa mwili kutoka kwenye udongo na mwishoni ndipoalipo mpulinzia pumzi na akawa nafsi hai.
>>Ndani ya nafsi kuna akili, na lakini ubongo upo kwenye mwili.  Ila kumbuka kuna uhusiano kati ya ubongo  na tutazama huko mbele.

2 Mungu anataka tujifunze nini kwa kutujulisha kuwa alitumia akili ili kuumba mbingu
_Mithali 3:19-20 Kwa hekima Bwana aliiweka misingi ya nchi; Kwa akili zake akazifanya mbingu imara; Kwa maarifa yake vilindi viligawanyika; Na mawingu yadondoza umande._
>>Sasa kwanini isitoshe tu kutuambia kuwa Mungu aliumba mbingu na nchi sasa kwanini biblia inaenda ndani kutueleza kuwa wakati mbingu inaumbwa Mungu alitumia kitu gani? Angali tena hiyo mistari.

>>Sasa kwanini Mungu anatupeleka jikoni, unajua ukienda hotelini unahitaji kujua tu kuwa chakula kimeiva na kianenda na ile thamani ya hela uliyolipa. Sasa anapokuja mpishi na kukueleza kuwa kwa kitunguu nilikaangiza mboga, au anaanza kukuambia namna chakula kilivyoandaliwa na namna vitu alikopata na vinavyoandaliwa, unaweza sema haina haja ya mimi kujua ila nataka kujua tu chakula kama kimeiva na kinaendana na ile hela niliyolipa.

>>Kumbuka hili, thamani ya chakula haipo kwenye chakula, ipo kwenye maandalizi ya chakula. Na ndio maana utaona hata cocacola hawatoi siri namna wanavyoanadaa cocacola maana wakikuambia hiyo furmula ina maana siku nyingine na wewe utatengeneza yaa kwako.  Kwa hiyo ndio maana wanabaki nayo wenyewe.

>>Sasa Mungu akikupa akili anataka uende jikoni ili ujue namna ya kuandaa hicho chakula. Angalia mistari ifuatayo
_Ayubu 38: 33 Je! Unazijua *amri zilizoamuriwa mbingu?* Waweza kuyathibitisha mamlaka yake juu ya dunia?_    >>Sasa ukiangalia ile mithali tunajua kuwa Mungu alitumia akili ili kuzifanya mbingu imara, na ile kusema  amri maana yake siyo sheria sasa katika Kiswahili tungesema kanuni yaani order au ordinance.  Maana yake zimewekwa kwa utaratibu na zimetengenezwa kwa mtazamo wa kiutekelezaji.

_Mathayo 5:34 lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu;_  sasa twende pole pole

_Hosea 2: 21-22 Tena itakuwa siku hiyo, mimi nitaitika, asema Bwana; nitaziitikia mbingu, nazo zitaiitikia nchi; nayo nchi itaiitikia nafaka na divai na mafuta; nayo yataiitikia Yezreeli. 

>>Sasa ukisoma kitabu cha Mwanzo 1:1 utaona biblia ikisema hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi, na haisemi nchi na mbingu fuata mtiririko kama biblia inavyosema,  kwa maana nataka kukupeleka jikoni kidogo  na mbingu anazozisema hapa sio hizi maana hizi biblia inazzita anga,  hapa nataka tuone mbingu ambazo ni kiti cha enzi cha Mungu  ambazo zina mamlaka juu ya nchi.

>>Hapo Mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi,  na anataka tuone namna akili ilivyokuwa ikifanya kazi katika uumbaji, si unakumbuka ile _Mithali 3:19 Kwa hekima Bwana aliiweka misingi ya nchi; Kwa akili zake akazifanya mbingu imara;_

Akili imegawanyika katika vitu vikubwa 3

1 Kutengeneza nia ya maisha
2 Kuetengeneza viwango vya maisha
3 Kutengeneza vipaumbele vya maisha

Zote hizi ziko hivyo kwa kufauatana na taratibu za amri.

Watu waliokoka wanapata shida sana wanaposoma maandiko na kuona walichokiona kwenye maandiko na namna maisha yao yalivyo wanapata shida sana, na kwa kuona wako kiroho tu wanajua kila kitu wanatapata hivyo hivyo ,hapana haiku hivyo, akili inatakiwa ifanye kazi au itumike katika vipaumbele vya maisha na vya KiMungu. _Mathayo 6:33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa._ na hawajui maana yake nini huu mstari maana wanakata kuelewa tu kiroho lakini Luka 24:45 ina kataaa maana inataka kwanza wafunuliwe akili zao ili waweze kuelewa maandiko.  Maana ili uelewe vizuri inabidi akili ishiriki.

*3 Akili zinafanya kazi kwa kutumia fikra ili ziweze kufanya majukumu yafuatayo*

~Uhusiano wa ubongo na akili ni kuwa ubongo unasimia maeneo mengi sana kufanya kazi, kwa hiyo kushindwa kwa ubongo kufanya kazi ya kusimamia eneo husika lile eneo nalo linaanza kupata shida.

~Kwa hiyo maeneo hayo yapo ndani ya akili kwa vipengele Fulani.

*a). Kuusaidia kuelewa mambo Kimungu*
_Luka 24:44-49 Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi. *Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko*. Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu. Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya. Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu._

>>Ilitakiwawapewe kwanza ufunuo wa Mungu.  Sasa kwa mfano Mtu akikuuliza ufunuo wa Mungu ana maana gani?

*b). Kukusaidia kupata ufahamu, kwenye Kingereza wameita understanding*

>>Maana yake unapata ufahamu wa neno na mazingira ya Kimungu., kwa hiyo ufahamu unakuwa juu yako ya maisha unayoishi, na mazingira na uhusiano na neno la Mungu. Kwahiyo ukielewa mambo haya hutaweza tena kucopy maisha ya mtu kwa sababu utakuwa unaishi maisha yako original. Kama unafikiri natania kawaulize polisi na watakueleza kuwa finger prints zako hazifanani na za mtu yeyote hapa duniani maana uko wewe mwenyewe.

>>Tulienda mkoa mmoja, na kulikuwa na hoteli nzuri sana  na tuliona hawauzi pombe yaani hamna pombe. Tulikuwa na hamu sana ya kutaka kujua huyu ni mtu wa aina gani aliyekubali  kufanya biashara ya hiteli bila ya kuweka pombe. Na walituambia huyo mtu sio mkristo ni wa dini nyingine, na tulipomfuatilia tuligundua kuwa yeye anakunywa pombe na hanywei hoteli kwake bali sehemu nyingine. Sasa huyu katengeneza aina ya maisha ambayo na yeye mwenyewe hayaishi.

*c). Kupanga matumizi ya kipato na rasilimali ulizonazo kwa kuzingatia vipaumbele vya*
     >>> Muda wa sasa na  baadae.
     >>> Mahitaji yako.
     >>> Mazingira.

_Mwanzo 41:32-33 Na ndoto ya Farao kwa vile ilivyokuja mara mbili, ni kwa sababu neno hilo Mungu amelithibitisha, na Mungu atalitimiza upesi. Basi, *Farao na ajitafutie mtu wa akili na hekima amweke juu ya nchi ya Misri*._

>>Sasa hapa Mungu alimsaidia Yusufu kuandaa mpango wa miaka 14  mfufulizo yaani kipindi cha uwingi na kipindi cha ukame.  Na maandko yanasema Yusufu alisema tafuta mtu mwenye akili na sio mtu wa kiroho. Mungu anatoa taarifa kupitia kwa Yusufu  na kuweza kupangilia  mahitaji kwa akili na hekima.

>>Na nataka uone namna akili ilivyofanya kazi.  _Mwanzo 41:37-38 Neno hilo likawa jema machoni pa Farao, na machoni pa watumwa wake wote. Farao akawaambia watumwa wake, Tupate wapi mtu kama huyu, mwenye roho ya Mungu ndani yake?_

>>Farao alijua anaweza akapata mtu mwenye akili na roho ya Mungu isikae ndani yake, bali lipata mtu wa akili na Roho ya Mungu iko ndani yake.  Kwahiyo jua kuwa Roho Mtakatifu ni mafuta na huwezi kujivunia kuwa umejazwa Roho Mtakatifu na hauna akili ina maana ni sawa sawa na kujivunia  mafuta bila ya kuwa na gari na pia gari bila mafuta halina kazi.

*d). Kukusaidia kupambanua mema na mabaya*

_Waebrania 5:14 Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima, *ambao akili zao*, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya._ *na akili kwa kuzitumia ndipo zinazoea* _2 Wakorintho 4:3-4 Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu._

>>Biblia inasema kuwa Mungu wa dunia hii anapofusha fikra za watu ili isiwazukie Nuru ya injili.  Akili ni Zaidi ya mawazo na kwa sababu hiyo akili zinaona.  Kazi ya akili ni kupambanua mema na mabaya.  Na Mungu aliwapo  waumba Adamu na Hawa alipowawekea mti wa mema na mabaya alikuwa wanatakiwa wajue kupambanua mema na mabaya lakini wao yaliyo mema wakaiona ni mabaya na mabaya wakona ni mema yaani walipata confusion. Biblia inasema katika _Mithali 23:7 a., maana aonanvyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo, au katika tafsiri zingine zinasema afikirivyo, au zingine zinasema awazavyo au atafakarivyo_

>>Shetani akipofusha fikra zako unakuwa na tabu sana maana Mungu anakumbia pita hapa unasema hapa unapita alipokukataza.  Mtu anayetegema akili siku zote ni *Hakubali kushindwa hata siku moja kwa sababu atafsiri kwa kutegemea akili peke yake* na *Hajui maana ya unyeyekevu ili kuoambanua mema na mabaya kwa msaada wa Roho Mtakatifu*.

>>Hapa utaelewa kwanini Mungu aliwapeleka wapelelezi 12 katika nchi ya Kanini kwa siku 40, siku zijazo ntakueleza ni kwanini siku 40  na waliporudi walitofautiana katika kutoa majibu. Ila wawili tu maana hawa ndio walikubali kumuweka Mungu katikati ya Fikra zao kuwa hata kama kuna majitu lazima hayawezi zuia ahadi za Mungu.

>>Nataka nikuulize swali jioni ya leo kuwa *Je unapopambanua maisha yako kujua mema na mabaya, na je akili zako zimelishwa kitu gani ili kujua namna ya kupambanua mema na mabaya?*

>>Wana wa Israel walikosea kupambanua na kujua vipaumbele vya Mungu na ndio maana wengine walikwama na hawakufika katika nchi ya ahadi. Ndio maana nauliza ni kitu gani unatumia kupambanua _Wakorintho 13:11-12 Nilipokuwa mtoto mchanga, nalisema kama mtoto mchanga, nalifahamu kama mtoto mchanga, nalifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto. Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana._

>>Sasa  kama hujabatilisha mambo ya kitoto inakuwa ngumu sana kwako kupambanua mambo vizuri,  maana kuwa wengine wanasema mimi ni wa Paulo na wengine wanasema mimi ni wa Apolo, biblia inasema wote hawa Fikra zao ni za Kitoto.  Kwa sababu wanapambanua maisha kidini  na dini kwao ndiyo kipaumbele.

>>Kwenye akili zako umepeleka kitu gani, je unapambanua mambo kisiasa, au kidini au kiumri au kwa kutumia neno la Mungu. *Unatumia nini kupambanua?*

>>Nilikuwa mkoa mmoja na kiongozi Fulani alinitambulisja kwao kuwa huyu ni Fulani Fulani, wakasema oooh, sawa huyu ndiye anayehubiri ila wakasema hapa haiwezekani maana Umri wako na Mambo unayoyasema ni tofauti sana.  Kwa sababu unajua mambo mengi sana na inaonesha umeishi maisha marefu sana hapa duniani.  Ila hao watu walipambanua kiumri. Ndio maana nakuuliza wewe unapambanua kwa kutumia nini?

>>Ndani yako je unaishi maisha ambayo ndiyo Mungu kakupangia, au umeshindwa kutumia akili na umeamua kuweka pembeni, leo nakumbia katika jina la Yesu rudi kwa Bwana  omba Mungu akusaidie namna ya kuoambanua maisha.

>>Huwa nikienda Israel nikipita katika bustani ile ya getsamane nakumbuka jinsi Yesua laivyokuwa anapambana na mwili wake na aina ya maisha ambayo Mungu aliyakusudia. Na akaanza kwa kusema mawazo yake baba  ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke. Lakini haikuwa mapenzi ya Mungu kikombe kimuepuke, na ahsante Yesu aliomba hadi Mwisho na alivuka. Chukia asingevuka wokovu tungeupata wapi. Hata mimi nikipita pale lazima nifanye toba kwa Mungu kuomba kama kunasehemu nimejiinua Mungu anisaidie au kuna sehemu nakwama Mungu anisaide. Sijajua kwa Upande wako umekwama wapi? Je nawewe umefika mahali unasema kikombe kikuepuke? Jion ya Leo nguvu za Mungu zimetufunika.. Mwambie Mungu akusaidie wapi kwenye akili zako.

>>Baada ya hapo yalifanyika maombi mazito san asana. Ukipata nafasi tembelea Youtube na utapata semina ya leo kwa kungalia link nilizoziweka hapo chini.

SEMINA IKO LIVE  KWA KUTUMIA NJIA ZIFUATAZO ZA INTERNET  KUANZIA SAA 9-12 JION

YouTube
https://www.youtube.com/channel/UC4p4lrpgpNd-9bHPgHJ4xWw

Ustream

http://www.ustream.tv/channel/mwakasegemanaministry

*Internet  radio*
www.mwakasege.org
www.kicheko.com

MAFUNDISHO ZAIDI.

FACEBOOK

https://www.facebook.com/Christopher-Diana-MwakasegeMana-Ministry-132462780111984/

Tovuti.
www.mwakasege.org

Summary za masomo haya na ya nyuma

http://www.gospelkitaa.co.tz/?m=1

http://www.kanisaforum.com/forums/Mafundisho-ya-Biblia/

VIPINDI VYA REDIO KILA WIKI
REDIO SAUTI YA INJILI MOSHI
Kila siku ya jumamosi na jumapili kuanzia saa tatu kamili usiku hadi saa nne usiku.

REDIO UPENDO YA DAR ES SALAAM.
Kila siku ya jumamosi na jumapili kuanzia saa tatu kamili usiku hadi saa nne usiku.

REDIO WAPO YA DAR ES SALAAM.
Kila siku ya Jumatano kuanzia saa tatu kamili usiku hadi saa nne usiku.

REDIO FARAJA YA IRINGA.
Kila siku ya jumamosi na jumapili kuanzia saa tatu kamili usiku hadi saa nne usiku.

REDIO FARAJA YA. SHINYANGA.
Kila siku ya jumamosi na jumapili kuanzia saa tatu kamili usiku hadi saa nne usiku.

REDIO UZIMA DODOMA
Kila siku ya jumamosi na jumapili kuanzia saa tatu kamili usiku hadi saa nne usiku.

REDIO VOICE OF TABORA (V.O.T)
Kila siku ya Jumatano kuanzia saa tatu kamili usiku hadi saa nne usiku.

KUNUA KANDA ZA SEMINA HII NA ZINGINE
http://www.mwakasege.org/nunua.htm na http://www.mwakasege.org/mawasiliano.htm

Ubarikiwe sana na Bwana Yesu.

🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏
*Felix Hezron Mbwanji*
*felixmbwanji@gmail.com*
*+255716918848*(whatsapp)
niandikie kwa maoni na ushauri na maboresho.

No comments:

Post a Comment