MOYO WA UTULIVU KATIKA FURAHA
Mungu amemuumbia mwanadamu upendo ndani yake ambao muda mwingi anatamani sana kueleza rafiki na ndugu zake kila kitu na jambo zuri linalotokea kwenye maisha yake, atukuzwe Mungu huyo huyo ambaye ameachilia Roho wake ndani yetu katika kutujulisha na kuturuhusu kusema kila jambo kwa watu, yeye awezaye kuruhusu useme kwenye mazingira mazuri anao uwezo wa kukuzuia usiseme njozi zako kwa kusudi maalumu.
Umechumbia/kuchumbiwa sehemu, kaa na Mungu tulia nalo katika furaha ya moyo wako, hadi utakapopata mpenyo wa kulisema hilo jambo, inawezekana kabisa halijafika muda wa kulisema kwa watu, ukisema umeharibu radha kabisa.
Mungu amekusemesha juu ya namna utakuwa siku za usoni kwenye utumishi ulio nao, kazi utakayo kuwa nayo, kanisa litakavyokuwa kubwa kwa utukufu wa Mungu, kaa nalo kwenye maombi, atamia hilo jambo hadi litakapokuwa limekomaa na kuwa tayari, kuku anapokuwa anaatamia mayai yake huwa hana urafiki wa kuku wengine kwa ukaribu wa kuwaamini sana kuku hao.
Yesu alikuwa na wanafunzi kumi na wawili lakini watatu tu ndiyo walikuwa wanajua siri nyingi za Yesu, wapi anapitia kwenye ugumu, na hata muda mwingine alikuwa akiwaeeleza jambo anawaambia msimwambie mtu yeyote kwa habari ya haya mambo.
Yusufu aliona ufahari sana kuwaeleza ndugu zake juu ya ndoto aliyoiota matokeo yake ndugu zake wakamchukia sana hata Ikafika hatua ya kupanga njama ya kumuua.
NOTE that;
1. Umechukiwa sana kwa sababu ya kufungua ukurasa kwa mtu au watu ambao siyo sahihi kwako na kuwaeleza ndoto zako, unaonekana unajidai wakati ndivyo ULIVYO
2. Si kila mtu anafurahia eneo ambalo Mungu kakuweka
3. Adui pia anatumia watu kukukwamisha
4. Jenga mazingira ya kumsikiliza sana Roho Mtakatifu juu ya nini cha kusema na nini cha kutokusema
5. Ukiona unapata ugumu kusema jambo lolote kwa watu unao waamini, acha hilo jambo haraka sana.
Nimekuombea Mungu akusimamishe katika kusudi lake mahali ulipo katika jina la Yesu
Good day much Love you all....
No comments:
Post a Comment