MVIVU
"Mtu yeyote anayekuambia juu ya hatari zilizoko kwenye njia yake kuelekea mafanikio anayoyataka, na anadai ndio sababu ya yeye kuacha kuchukua hatua kuelekea mafanikio, MTU HUYU NI MVIVU"
(Mithali 22:13).
"Mtu yeyote ALIYEFUNGA NDOA NA GODORO, anafanya kazi ya kugeuza mbavu zake, kama mlango unavyogeuka kwenye bawaba, MTU HUYU NI MVIVU"
(Mithali 26:14).
"Mtu anayependa kusukumwa sukumwa, kusimamiwa simamiwa, kuelekezwa elekezwa, kuambiwa ambiwa mambo ambayo alipaswa kujiambia, kujielekeza, kujisukuma, kujisimamia, MTU HUYU NI MVIVU"
(Mithali 6:6-8).
"Mtu asiyefikiri kuhusu kesho, na kuweka mikakati ya kuikabili hiyo kesho, anasubiri vitu vitokee bila mipango na maandalizi, MTU HUYU NI MVIVU"
(Mithali 6:6-8).
"Mtu yeyote ambaye mambo yake yako shaghalabaghala, hayana mipangilio, hayana unadhifu, uzuri na ubora, MTU HUYU NI MVIVU"
(Mithali 24:30-34).
"Mtu yeyote anayeuhurumia mwili wake, na anapenda kujihurumia hurumia, badala ya kuutesa mwili na matakwa yake ya muda mfupi, MTU HUYU NI MVIVU"
(Mithali 20:4).
Mtu yeyote ambaye ukijaribu kumulekeza yampasayo ili afanikiwe, anajitia mjuaji na anakupa sababu nyingi za kwanini haiwezekani, badala ya kwanini aweze, MTU HUYU NI MVIVU
(Mithali 26:16).
NAIAMURU ROHO CHAFU YA UVIVU IKUTOKE KWA JINA LA YESU.
No comments:
Post a Comment