MPIRA UMEKWISHA YANGA 1 ZANACO 1
TATHIMINI KWA YANGA SC
George Lwandamina kaianza vyema mechi kwa hesabu za kimbinu na kiufundi. Licha ya kasi na matumizi makubwa ya nguvu aliwaweza kwenye marking na kuwatoa mchezoni kwa kuwatumia Yondani , Zulu , Kamusoko na Ngoma .
Timu imetengeneza nafasi nyingi za kufunga sema utulivu wa forward line ya Yanga kwenye finishing ilikuwa tatizo ukiacha nafasi moja waliyoipata na Msuva kufunga bao dakika ya 39. Ni goli lililotafutwa vizuri kimbinu kazi ikianzia kwa Ngoma akirudi chini kama Play maker na kumpasia Zulu wing ya kulia ambaye kwa utulivu mkubwa anamtengea Msuva ndani ya 18 na yeye akionesha kuwa yupo matured anatengeneza goli zuri.
Nini kimewafanya Yanga kushindwa kulinda goli?
Kwa macho mepesi unaweza mtupia lawama kocha kwa mabadiliko aliyoyafanya kwa kuwatoa Ngoma na Kamusoko na kuwaingia Emanuel Martini na Juma Mahadhi na ndipo Zanaco walipoanza kuja kwa kasi na kutengeneza goli.
Kwanza kabisa ni lazima tukubali jambo moja kabla ya kumtupia lawama kocha . Lazima tuwe na mtazamo sahihi katika kufikiri na kutoa majibu sahihi. Yanga SC kimbinu na kiufundi ina wachezaji wengi ambao ni averaged players . Wachezaji kiwango cha wastani ambao wanakosa basics nyingi kimbinu na kiufundi na hili si kwa Yanga tu ni sehemu kubwa ya nchi yetu kwa sababu hatuna misingi mizuri huko chini.
Ngoma ameingia katika mechi hii akiwa hayupo sawa kwa zaidi ya asilimia 50 lakini 50 zilizobaki ndizo alizotusaidia kuwatuliza wazambia kule mbele na kuanzisha move ya goli. Jiulize asingecheza kabisa ingekuwaje?!. Kocha kamtoa nje baada ya hali yake kuwa tete na kuanza kucheza kwa woga kwa hofu ya kuumia. Hofu yake ilianza kuwapa amani Zanaco na kucheza free. Kocha kamtoa nje na kumwingiza Emanuel ili kuendeleza tempo ya mchezo lakini Martin kapoteza nafasi nne za wazi kwa kukosa utulivu na umakini kimbinu . Lwandamina aingie kucheza ?
Kamusoko majeruhi wa mechi ya watani wa jadi. Leo kaanza kama kiungo mshambuliaji akiwa bado hajapona sawa . Na imelazimika kupangwa baada ya Tambwe kuwa bado majeruhi na Niyonzima kuchelewa mazoezi . Amefanya mazoezi siku mbili tu akikosekana zaidi ya siku sita ! anatoa wapi match fitness?! Apangwe aitwe muhujumu tena ?! au kuvunja morali ya waliotoka jasho juma zima?! Kumpa nafasi Kamusoko GL alicheza vyema kamari lakini kutoneshwa na kuanza kucheza kwa hofu ilimlazimu kocha kumtoa .
Shida moja ya Mahadhi hajatambua kama GL anamwamini na anatamani afanikiwe. Mabadiliko yake kwa Kamusoko yalilenga vitu viwili ambavyo yeye imekuwa tatizo kuvitimiza. Kwanza ku " mantain " mashambulizi na kuhakikisha mpira mbele unakaa na cha pili kuhakikisha muunganiko wake na viungo chini yake unaimarishwa katika " direct play ". Mahadhi kaingia akawa flat & floppy na kuwaruhusu Zanaco kuwa na mipango mizuri toka chini hali iliyofanya kiungo chote cha Yanga kuvamiwa na kumtoa kabisa mchezoni Zulu kwenye mipango ya kushambulia na kujikuta wakijikusanya kati na Yondani bila mwelekeo.
Jicho la GL likaamua kumtoa Zulu na kumleta Kaseke; kwanza awape back up Mahadhi na Yondani pili ajaribu kuisukuma timu mbele . Kidogo hii ilisaidia.
Bado Yanga ina nafasi ya kushinda ugenini endapo hawa majeruhi watakuwa safi na Haruna kucheza . Lakini timu inahitaji " build up " kubwa kiufundi kwa aidha wachezaji kubadilika na kucheza kama matured players wanaoweza kutafuta goli na kulilinda.
Narudia tena tazameni timu yenu , mahesabu wanayotumia waalimu na uwezo wa mchezaji mmoja mmoja kabla ya kumlaumu mwalimu.
Kwanini Zulu hajatumika kama kiungo mkabaji?
Endapo Kamusoko angekuwa vyema kwa asilimia 100 . Yaani mzuri kwenye battling bila hofu ya kujitonesha ? Ni dhahiri kocha angeanza na Zulu chini , Kamusoko juu , Ngoma tisa na kumi Chirwa na pembeni Kaseke lakini Kamusoko na Ngoma wameingia kama kamari hivyo lazima nyuma yao uwape mtu wa back up . Mtu ambaye anaweza kufuta makosa yao kwenye marking pia kuwafungulia njia ili wacheze soka kwenye open space ndio maana Zulu akapangwa juu kama box to box na chini yake Yondani . Ni kama kocha alipandisha ukuta wa marking kwa juu ya Nadir na Bossou kumweka Yondani na amefanya kazi nzuri kabla ya kiungo chao kuvurugwa kwa mabadiliko.
Mtazamo wangu
Saturday, March 11, 2017
MPIRA UMEKWISHA YANGA 1 ZANACO 1 HII NDIYO TATHIMINI KWA TIMU YANGU DAR- YOUNG AFRICAN
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Sema na Safari ya Ligi ya Mabingwa imeishia hapo sidhani kama mtawafunga kwao,coz mmeshindwa kuutumia vizuri uwanja wa nyumbani. Karibuni kombe la Shirikisho.. "Hakuna maneno kwenye khanga!!!!".. …
ReplyDeleteBab wacha maneno ww ona sasa
DeleteUmefanya mpaka uongo ukawa kweli
ReplyDelete