YAJUE MAMBO AMBAYO MKAKA YEYOTE ANAYOYAHITAJI.
Madada (Wanawake) wengi wanahisi wanawafahamu sana wakaka, sikatai ila wengi wao wanawafaham kwa sehemu tu, ukitaka kuishi na mtu vizuri jenga nidhamu ya kumfahamu, na huwez kumfaham bila kwenda kwa aliyemuumba kwanza katika kitabu cha mwanzo, tambua ni vitu gani Mungu aliviweka ndani yake.
Mkaka yeyote yule, ni mshamba au mjanja, ni msomi au mpoli poli, ameokoka hajaokoka, ni mfupi au mrefu, ni mweupe au mweusi, ana kitambi au hana, wote hawa kwa makundi yao wanahitaji sana sana kitu kinaitwa KUHESHIMIWA hilo jambo likikosekana, utaona mkaka anaanza kuwa na hasira kama mbogo, why anatetea nafasi yake kuporwa, nafasi ipi nafasi ya kunyimwa heshima yake.
Ukiona unakaa na mkaka mwezi mmoja ghafla anapotea kimya kimya, chunguza maneno yako kwake, huyo siyo mdada mwenzako ujue, unamzodoa amekuwa mdogo wako? amekuwa mdada mwenzako? silaha ya mwanamke mwenye akili ya kulinda nyumba yake yuko makini sana katika kufungua kinywa chake.
Hata kama Yesu kaongea na wewe mengi juu yako katika mahusiano yako, unahitaji nidhamu sana katika kuongea nae, wengi wameachwa kwa ajili ya dharau na kiburi, mdada yeyote mwenye kiburi chunguza mwisho wake, ni kuachika kila kukicha
Ndiyo maana unaweza kuona wakaka wengi waliookoka utakuta wanammendea mdada mmoja kwenye fellowship, why, kitu gani wameona, HESHIMA ukiona wakaka hawakatizi kwako cha kwanza omba Mungu aondoe mtazamo wanaouona juu yako ya kiburi ili akupe hekima inayoleta nidhamu ya heshima kwa mkaka, huamini endelea na kiburi chako uone kama kuna mkaka atapata shauku ya kuwa na wewe.
Mungu awabariki sana wadada wote wenye heshima, mjue uzuri ni ubatili bali mwanamke amchaye Bwana huyo ndiye atakayesifiwa .
Somo ni refu, sijaanza kufundisha hapo, huo ni utangulizi tu.
Chuoni huwa tunauliza watu waliotutangulia juu ya taarifa muhimu za mwl, nini huyo mwl anataka, je huwa anatabia za kubana course work? je anapenda uandike sana maelezo? au hataki maelezo sana? je anatoaga mekapu? yote hiyo ni ili kuenda naye vizuri baada ya kumfahamu, ninachohofia wengi hukumbuka shuka wakati wa asubuhi, means TOO LATE, fahamu sana mambo ambayo mkaka anayahitaji, mkaka mbona utafurahia tuuu? yajue tu, leo nimeongelea point moja tu. Nitawaletea point wakati mwingine poin nyingine .
No comments:
Post a Comment