HAMORROIDS AU BAWASIRI
Bawasiri ni mojawapo ya tatizo ambalo mara nyingi linapotokea humfanya mtu kuwa na aibu kuelezea au kwenda hospitali ili kupata tiba sahihi. Bawasiri au hemorrhoids husababishwa na kuvimba kwa mishipa ya damu aina ya vena katika eneo la mfereji wa haja kubwa.
AINA ZA BAWASIRI
NJE
Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huweza kuambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina kitaalamu inaitwa Thrombosed hemorrhoid.NDANI
Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu na wengi huwa hawatambui kuwa wanatatizo hili.
Aina hii imegawanyika katika mainisho yafuatayo:Daraja I- Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
Daraja II- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja III- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja IV- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.
Je bawasiri husababishwa na nini?
BAWASIRI HUSABABISHWA NA NINI?
Bawasiri husababishwa na;
Tatizo sugu la kuharishaKupata kinyesi kigumuUjauzitoUzito kupita kiasi (obesity)Kupenda kufanya ngono ya njia ya haja kubwa (anal sex)Kwa ujumla mambo yanayo ongeza shiniko katika tumbo.Umri mkubwaDALILI ZA BAWASIRI
Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia (hematochezia)Maumivu au usumbufuKinyesi kuvujaKijiuvimbe katika eneo la tundu la haja kubwaNgozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwaKujitokeza kwa kinyama (bawasiri) wakati wa haja kubwa
MATATIZO YANAYOWEZA KUTOKEA KUTOKANA NA BAWASIRI
Upungufu wa damu mwilini (Anemia)Strangulated hemorrhoids
VIPIMO NA UCHUNGUZI
Digital rectal examinationKipimo cha njia ya haja kubwa (Proctoscope)Kipimo cha utumbo mpana (Sigmoidoscope)
MATIBABU
Matibabu hutegemea na hali na aina ya Bawasiri
Rubber band ligation - Hapa mishipa hufungwa na rubber band ili kuzuia damu kwenda kwenye eneo liloathirika, na hutumika kwenye aina ya ndani ya bawasiri.Sclerotherapy- Hapa kemikali huwekwa kwa njia ya sindanoCoagulation (infrared, laser and bipolar)Upasuaji; Hemorrhoidectomy
Stapled hemorrhoidopexy
NJIA ZA KUZUIA BAWASIRI
High fibre diet, kula mboga za majani, matunda, na nafaka kwa wingi.Kunywa maji mengi kwa siku (glasi sita had nane kwa siku)Punguza kukaa kwa muda mrefu sana hasa ukiwa chooni, kwa sababu unaweza kuongeza shinikizo katika mfereji wa haja kubwa
DAWA YA MARADHI YA BAWASIRI ZA AINA ZOTE
Ndugu zangu kichwa hapo juu chaweza kumfanya mtu ajiulize swali, je bawasiri zipo za aina ngapi?
Jawabu ni kuwa bawasiri zipo za aina mbili.
Aina inayotembea (Yaani ikitoka ndani na kurudi) Aina inayosimama (Yaani kinyama kinachoota kwenye dubuni).Sasa bawasiri zote hizi tiba yake n hizi zifuatazo
Kitunguu swaumu (Vijiko vitatu vya chakula)Asali (Nusu lita)Tangawizi (Vijiko vitatu vya chakula)Mbegu za Figili (CELERY) - (Vijiko vitatu vya chakula)Matumizi: Madawa haya lazima yapimwe kwa idadi hiyo yakiwa tayari yamekuwa unga, kisha changanya pamoja, na dozi yake ni kama ifuatayo;Kijiko kimoja cha unga wa madawa haya utakilamba asubuhi, mchana utafanya kama hivyo tena kisha jioni yaani (1 X 3) kwa muda wa siku saba hadi kumi na moja (7 - 11).
No comments:
Post a Comment