Friday, January 19, 2018

  RATIBA NGUMU NI NYEPESIKWA MAFANIKIO

              RATIBA NGUMU NI NYEPESI
       KWA MAFANIKIO.

Ni rahisi kusikia watu wanasema jamaa anaratiba ngumu au pamoja na ratiba yake lakini bado amekuja na huku au bado amefanya na hili. Wanasahau  kuwa ratiba ngumu ni nyepesi kwa mafanikio na ratiba nyepesi ni ngumu kwa mafanikio. Tunatofautiana sana katika ratiba zetu kutokana na utofauti wa maono na vipaumbele vyetu. Wakati wengine wanatafuta vitu vya kufanya lakini wengine kupata muda wa kupumzika ni muujiza. Na ukitaka kukorofishana nao ingilia muda wao wa kupumzika. Maana wanauheshimu.

Unapatikana kiurahisi kwa sababu huna cha kufanya ratiba yako ni nyepesi sana na inawezekana pia huna wewe ni bora siku iende ulale uamke. Cha ajabu wengi tunapenda mafanikio lakini gharama za mafanikio hatutaki kuzilipa. Kila siku watu wanakukuta katika kijiwe na wanakuacha. Haujui ni siku ipi kwako imebana na siku ipi una angalau nafasi. Siku zote kwako sawa.
-Ratiba ngumu sio ile ya kubandika ukutani na kubaki unaitazama.
-Ratiba ngumu sio ile haupatikani na unachokifanya hakionekani kwako wala kwa waliokuzunguka.
-Ratiba ngumu sio ile unakosa hata muda na familia yako.
-Ratiba ngumu sio ile unakosa hata muda wa kuingia nyumba za ibada.
-Ratiba ngumu sio ile unakosa hata muda wa kupumzika.
-Ratiba ngumu sio ile unakosa hata muda wa kula bata na rafiki zako.
-Ratiba ngumu inajumuisha yote hayo niliyotaja pamoja na kuacha alama kwa jamii yako kwa yale unayoyafanya.

Mafanikio mengi ni matokeo ya jitihada na bidii kubwa katika yale mtu anafanya. Jitihada hizo ndizo zinampelekea kuwa na ratiba ambayo akiifuta na kufanya kazi kwa bidii inayotakiwa itamletea mafanikio aliyotarajia kuyapata au kuyafikia. Akili inaposhughulishwa na mambo mengi yaliyopangiliwa inakuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri na kutatua mambo. Ndio sababu waingereza wanamsemo wao wanasema ' ukitaka jambo lako lifanywe haraka na kufanikiwa mpe mtu busy kuliko wote alifanye' wanaamini hivyo sababu wanaamini atafanya haraka ili aweze kuendelea na mambo yake lakini atalifanya vizuri ili asije ambiwa kurudia kulifanya maana atakuwa anapoteza muda kurudia kufanya jambo hilo.
Ikague ratiba yako ni nyepesi au ngumu. Je itakufanya ufanikiwe katika malengo uliyojiwekea. Ukiona ratiba yako imebana lakini nje ya malengo uliyojiwekea ujue siyo ratiba ngumu hiyo. Ni nyepesi sana.

#Kila kitu kinatengenezwa#
JIFUNZE KUJIFUNZA
@Kuwa Ni Kufanya&

No comments:

Post a Comment