Monday, February 26, 2018

KUWA NA MOYO WA UTULIVU KATIKA FURAHA

MOYO WA UTULIVU KATIKA FURAHA

Mungu amemuumbia mwanadamu upendo ndani yake ambao muda mwingi anatamani sana kueleza rafiki na ndugu zake kila kitu na jambo zuri linalotokea kwenye maisha yake, atukuzwe Mungu huyo huyo ambaye ameachilia Roho wake ndani yetu katika kutujulisha na kuturuhusu kusema kila jambo kwa watu, yeye awezaye kuruhusu useme kwenye mazingira mazuri anao uwezo wa kukuzuia usiseme njozi zako kwa kusudi maalumu.

Umechumbia/kuchumbiwa sehemu, kaa na Mungu tulia nalo katika furaha ya moyo wako, hadi utakapopata mpenyo wa kulisema hilo jambo, inawezekana kabisa halijafika muda wa kulisema kwa watu, ukisema umeharibu radha kabisa.

Mungu amekusemesha juu ya namna utakuwa siku za usoni kwenye utumishi ulio nao, kazi utakayo kuwa nayo, kanisa litakavyokuwa kubwa kwa utukufu wa Mungu, kaa nalo kwenye maombi, atamia hilo jambo hadi litakapokuwa limekomaa na kuwa tayari, kuku anapokuwa anaatamia mayai yake huwa hana urafiki wa kuku wengine kwa ukaribu wa kuwaamini sana kuku hao.

Yesu alikuwa na wanafunzi kumi na wawili  lakini watatu tu ndiyo walikuwa wanajua siri nyingi za Yesu, wapi anapitia kwenye ugumu, na hata muda mwingine alikuwa akiwaeeleza jambo anawaambia msimwambie mtu yeyote kwa habari ya haya mambo.

Yusufu aliona ufahari sana kuwaeleza ndugu zake juu ya ndoto aliyoiota matokeo yake ndugu zake wakamchukia sana hata Ikafika hatua ya kupanga njama ya kumuua.

NOTE that;

1. Umechukiwa sana kwa sababu ya kufungua ukurasa kwa mtu au watu ambao siyo sahihi kwako na kuwaeleza ndoto zako, unaonekana unajidai wakati ndivyo ULIVYO

2. Si kila mtu anafurahia eneo ambalo Mungu kakuweka

3. Adui pia anatumia watu kukukwamisha

4. Jenga mazingira ya kumsikiliza sana Roho Mtakatifu juu ya nini cha kusema na nini cha kutokusema

5. Ukiona unapata ugumu kusema jambo lolote kwa watu unao waamini, acha hilo jambo haraka sana.

Nimekuombea Mungu akusimamishe katika kusudi lake mahali ulipo katika jina la Yesu

Good day much Love you all....

ZITAMBUWE SIKU HATARI ZA KUPATA MIMBA KWA MWANAMKE

Ili kufahamu vizuri ni siku zipi ni hatari kwa mwanamke kupata mimba,ufahamu thabiti kuhusu mzunguko wa hedhi[menstrual cycle] ni jambo la muhimu sana.

Kwa wastani,mzunguko wa hedhi ni siku 28.
Mzunguko wa hedhi unaanza kuhesabiwa kuanzia siku ya kwanza mwanamke anapoanza ku bleed(label it as day one).

MZUNGUKO WA HEDHI WA KAWAIDA UNA SIFA MADHUBUTI[CHARACTERISTICS OF NORMAL MENSTRUAL PERIOD]

1.IDADI YA SIKU KATIKA MZUNGUKO MMOJA(cycle length)
Kwa kawaida idadi ya siku katika mzunguko ambazo huhesabika kama ni mzunguko wa kawaida ni siku 21 hadi 35 (ambapo hapo ndipo unapata wastani wa siku 28 yaani [(21+35)÷2].
Kwahiyo ndugu msomaji usikariri kuwa mzunguko wa kila mwanamke una siku 28,hiyo ni big no.wengine wana siku 27,wengine 25,wengine 35,wengine 29.

2.SIFA YA PILI NI UWIANO WA IDADI YA SIKU ZA MZUNGUKO KATI YA MZUNGUKO MMOJA NA MWINGINE(REGULAR VS IRREGULAR CYCLES) .
Hii ni miongoni mwa changamoto kubwa sana katika suala zima la ngono kwani inaweza kuwa vigumu kuzitambua siku hatarishi kwa mwanamke kupata mimba.
Ili tuseme mwanamke anamizunguko ya hedhi iliyo sawa[regular cycles],idadi ya siku za mizunguko ya hedhi isitofautiane kwa zaidi ya WIKI MOJA[7 days].
Kwa mfano,kama mwezi wa kwanza aliona siku zake baada ya siku 28,mwezi wapili akaona baada ya siku 30,mwezi wa tatu akaona baada ya siku 35 na wanne akaona baada ya siku 21,bado mzunguko wake uko kwenye uwiano mzuri[regular cycle] kwasababu mzunguko mmoja na mwingine haujatofautiana kwa zaidi ya siku 7.
Usikariri kuwa siku za mzunguko kwa kila mwanamke ni siku 28,hiyo ni big NO.Hiyo 28 ni wastani tu.
Wengine wana bleed kila baada ya siku 21,wengine25 wengine,29,wengine 35 na bado tunasema mizunguko yao bado ni regular[uwiano sahihi].
Pia tambua ya kuwa si lazima idadi ya siku katika mzunguko mmoja ilingane na mzunguko mwingine kwa mwanamke huyohuyo,kwa mfano usitarajie kuwa kama mwezi march ame bleed baada ya siku 28 na mwezi april pia ata bleed baada ya siku 28,sio lazima iwe hivyo lakini pia inaweza tokea.
Kwa mfano mwanamke mzunguko huu anaweza kuona siku zake baada ya siku 28,mzunguko unaofuata baada ya siku 27,mzunguko mwingine baada ya siku 30,mzunguko mwingine baada ya siku 29,mzunguko mwingine baada ya siku 25 na bado yuko kwenye uwiano sawa(tofauti si zaidi ya siku 7).

3.IDADI YA SIKU ZA KUBLEED[MENSTRUAL PERIOD]
Usichanganye kati ya menstrual period na menstrual cycle,hivi ni vitu viwili tofauti kabisa.
Siku ya kwanza ya kubleed ndo siku tunayoanza kuhesabu mzunguko wa hedhi[day one],sio siku ya kumaliza ku bleed. Kwa kawaida idadi ya siku za ku bleed ni kati ya siku 3 hadi 7,kila mwanamke ana idadi yake kati ya hizo.

4. Sifa ya mwisho ya mzunguko wa hedhi ni WINGI WA DAMU inayotoka wakati wa hedhi[amount of menstrual blood],ambapo mwanamke anaweza ku bleed kawaida[normal bleeding] au ku bleed sana[heavy bleeding].

ILI KUZIFAHAMU VIZURI SIKU HATARI KWA MWANAMKE KUPATA MIMBA HEBU TUANGALIE KIDOGO JINSI MAYAI YANAVYOKOMAA NA KISHA KUTOLEWA KWENYE OVARY.
Tufahamu mzunguko wa ovary(ovarian cycle).
Mzunguko wa ovary[ovarian cycle) ndio unaoleta mabadiliko katika mfuko wa uzazi(menstrual cycle).
Mzunguko wa ovary una hatua zifuatazo
Follicular phase,ovulation na luteal phase.

1.FOLLICULAR PHASE: Sehemu hii ya mzunguko huanza siku ya kwanza ya mwanamke ku bleed mpaka yai linapokuwa limekomaa[graafian follicle)
Mayai ya mwanamke huanza kutengenezwa wakati akiwa tumboni mwa mama.
Mpaka kufikia balehe [puberty],mwanamke anakuwa na mayai yapatayo 400,000 ndani ya ovary,mayai haya huwa katika hatua ya uchanga[primary oocyte].

2.OVULATION; katika hatua hii ya mzunguko wa ovary,yai lililokomaa[graafian follicle] hutoka kwenye ovary na kuingia kwenye mirija ya fallopian.
Sasa tutaitambuaje siku ya yai kutoka[ovulation]?.
Kiuhalisia ni ngumu kujua siku halisi yai lilipotolewa lakini tunaweza kuzitambua siku nyeti ambazo zitatupa nafasi kubwa ya kutokulikosa yai ndani ya siku hizo.Fuatilia hapo chini.

3.LUTEAL PHASE : hii ni sehemu ya mzunguko wa ovary ambayo huanza baada ya yai kutoka[ovulation] na kuishia kabla ya kuanza ku bleed[mwanzo wa mzunguko mwingine).
ZINGATIA HAPA, idadi ya siku kati ya ovarian cycle na menstrual cycle ni sawa[mfano,28,30,35,25).
Idadi ya siku katika luteal phase ni sawa kwa mizunguko yote na ni siku 14.

ANGALIA HESABU HII RAHISI
Folicular phase +luteal phase =Idadi ya siku katika mzunguko[the cycle length).
Lakini tayari tumeshajua luteal phase ni constant,haibadiliki,[ni siku 14 katika kila mzunguko].ovulation phase hapo iondoe maana ovulation hutokea masaa machache tu.
Sasa ili kuipata siku ya ovulation,tunachukua idadi ya siku katika mzunguko mmoja - idadi ya siku katika luteal phase,ambayo haibadiliki[14 days].
Kwa mfano kwa mwanamke mwenye mzunguko wa siku 28,kuipata siku ya ovulation tunachukua 28-14 tunapata 14,kwahiyo kutoka siku ya kwanza mwanamke alipoanza kubleed ni siku ya 14 ndipo yai linakuwa tayari kurutubishwa.
Kwa mwenye mzunguko wa siku 30, tunachukua 30-14(luteal phase)=16,kwa hiyo mwanamke mwenye mzunguko wa siku 30,ovulation inauwezekano mkubwa wakutokea siku ya 16 na si ya 14(kuwa makini hapo).
Yule mwenye mzunguko wa siku 35 ,ovulation day ni 35-14 = 21,kwa hiyo kwa mwanamke mwenye mzunguko wa siku 35,ovulation ina nafasi kubwa ya kutokea siku ya 21 na si ya 14.
Sasa baada ya kuijua siku ya ovulation lazima uwe makini na siku zinazokaribiana na siku ya ovulation kwani nazo ni siku hatari pia.
KWANINI?

Mbegu ya kiume inauwezo wa kuwa hai hadi masaa 48 (2 days) tangu shahawa zimwagwe[ejaculation] na yai lina uwezo wa kuwa hai hadi masaa 24[one day] tangu lilipotoka kwenye ovary.
Kwaiyo kama mwanaume akijamiiana na mwanamke siku mbili kabla ya yai kutolewa kwenye ovary, mbegu inaweza kuwa hai bado na kutungisha mimba endapo yai litatolewa ndani ya siku mbili zijazo kwa mfano kama siku ya ovulation ya mwanamke ni siku ya 14, mwanamke akijamiiana na mwanaume siku ya 12, uwezekano wa kupata mimba ni mkubwa.
Kadhalika kama mwanamke ametoa yai siku ya 14 kisha akajamiiana ndani ya masaa 24 mbele, pia anaweza kupata mimba kwasababu kipindi mbegu zinamwagwa zinaweza kulikuta yai bado lipo hai na kutungisha mimba.
Kwa ufupi,ni siku tatu tu ndizo hatarishi sana kwa mwanamke kupata mimba,yaani,siku mbili kabla ya ovulation na ndani ya masaa 24 baada ya ovulation[narrow but dangerous window].
Kwa kuongezea,kipindi cha ovulation mwanamke anapata nyege kali sana kwasababu ni kipindi ambacho kuna homoni fulani[androgens] ambazo huchochea nyege huzalishwa kwa wingi. Pia kipindi hicho cha ovulation au karibia ovulation joto la mwili la mwanamke hupanda,anajihisi mwili kuchemka tofauti kidogo na ilivyo kawaida yake.

SASA BASI KWA KUWA NIMESEMA HATUWEZI KUWA NA UHAKIKA WA 100% WA SIKU YA OVULATION NDO MAANA HUWA TUNATUMIA KANUNI YA KUEPUKA NGONO KWA KIPINDI CHA WIKI NZIMA[7 DAYS] AMBAZO NI SIKU ZILIZO KARIBU SANA NA SIKU YA OVULATION KWA WALE WANAOTUMIA CALENDER METHOD.

Mfano,kama una mzunguko wa siku 30, kuipata siku ya ovulation chukua 30- 14=16,kwa hiyo siku ya ovulation ni ya 16 tangia ulipoanza kuona damu siku ya kwanza.sasa kama ni siku ya 16,ondoa siku nne kabla ya hiyo siku ya ovulation.kwahiyo kuanzia siku ya 12 hapo,acha ngono.
Pia jumlisha siku 3 mbele,ambapo mwanamke atatakiwa kuanza ngono kuanzia siku ya 19 huko ili kuepuka mimba.

Friday, January 26, 2018

JE, NIINGIE KWENYE MAISHA YA NDOA NA NANI?

JE, NIINGIE KWENYE MAISHA YA NDOA NA NANI?

Wengi limekuwa jambo gumu sana kutaka kujua aingie kwenye maisha ya mahusiano na ndoa bdae na mtu gani, unisikilize itakusaidia.

1. Hakikisha mtu huyo anamcha BWANA.

Wewe siyo Yesu hadi uokoe, si swala la kuingia na mtu asiyemcha BWANA ukidhani uko salama, maandiko yanasema tusifungiwe nira na mtu asiye amini.

Kuamini nini, kuamini imani ya Kristo Yesu

Neema ya wokovu bado ipo, utashangaa utakapoamua kukubali kuiingia kwenye maisha na mtu asiyeamini imani yako ghafla ameshakuweka ndani anakugeukia, anakwambia kuanzia leo hakuna kwenda kanisani, anakuchekea leo, kesho atakugeuka, moyo wa mwanadamu kama haumjui Mungu ni hatari sana...

Tukumbushane kidogo hapa wapendwa "Kilichomfanya Yusufu amkimbie yule mama mke wa potifa bila kufanya nae dhambi, ilikuwa ni neema ya kumjua Mungu iliyokuwepo juu ya Yusufu", Sasa fikiria ndiyo imemtokea boyfriend wako ambaye hamjui Mungu, kitu gani kitatokea..? (Jitafakari moyoni mweyewee hata usichekee)

Weit my friend God's Fearful relationship itakusaidia kukutunza hata kama mwili utainuka, utastahimili usimtende Mungu dhambi kwa sababu tu ya neema ya kuwa na hofu ya Mungu baina yako na mtu uliyepo kwenye mahusiano, ila kama mmoja hofu ya Mungu haipo, uwe na uhakika hamtaweza kustahimili, trust me.

Mabinti wengi wanaomjua Mungu waliopo makanisani, asilimia kubwa hawako tayari kuolewa na vijana wa kanisa, why,.

Vijana wa kanisani wanaonekana washamba sana, watu wa mabwanga, asante Yesu nilizungumza sababu zinazopelekea wakaka kuachika sana, likiwemo hilo.

Suluhisho.

Mueleze kwa hekima, vaa shati linalokutosha vizuri, vaa suluari zinazokuenea vzr

Akikataa, tulia kwanza, rudi tena, maana ni wabishi kubadili kwa haraka haraka, muombe Mungu akusaidie hadi aelewe.

Nia yangu ni hii, usimuache mkaka kisa anavaa mabwanga, ndiyo maana upo umsaidie awe smart, ili uanze kumtambulisha bila aibu kwa marafiki zako.

2. Mwenye kujua nini anapaswa kufanya kwa mwenzake kutimiza kusudi la yeye kuwa na mwenzake.

3. Aliye tayari kujifunza, kuongozwa na mwanaume huyo, kama haupo tayari kujifunza kwake na kuongozwa naye kama kiongozi wa familia, usikubali akuoe, muache atafute mwingine.
Usikubali kama haupo tayari kuwajibika kwake​,
Usikubali kama unaona anapwaya kwenye vigezo vyako, yaani siyo shauku ya moyo wako, usikubali kuwa naye, muache atafute mwingine​.

4. Hakikisha amani ya moyo wako kutoka ndani kabisa imekubali kwenda na mtu huyo, yaani mkaka huyo, usiingie nae kisa ana kibanda cha chipsi mayai, usikubali kisa ana kioski, usikubali kisa ana salon ya wadada, usikubali kisa ana gari, usikubali kisa ana nyumba, upendo haujengwi kwa vitu, uwe na uhakika ndani yako uhalisia unakataa, upendo unakuja automatic, love without any reason will sustain your relationship.

Friday, January 19, 2018

YAJUE MAMBO AMBAYO MWANAUME YEYOTE ANAYOYAHITAJI.

YAJUE MAMBO AMBAYO MKAKA YEYOTE ANAYOYAHITAJI.
Madada (Wanawake) wengi wanahisi wanawafahamu sana wakaka, sikatai ila wengi wao wanawafaham kwa sehemu tu, ukitaka kuishi na mtu vizuri jenga nidhamu ya kumfahamu, na huwez kumfaham bila kwenda kwa aliyemuumba kwanza katika kitabu cha mwanzo, tambua ni vitu gani Mungu aliviweka ndani yake. 

Mkaka yeyote yule, ni mshamba au mjanja, ni msomi au mpoli poli, ameokoka hajaokoka, ni mfupi au mrefu, ni mweupe au mweusi, ana kitambi au hana, wote hawa kwa makundi yao wanahitaji sana sana kitu kinaitwa ​KUHESHIMIWA​ hilo jambo likikosekana, utaona mkaka anaanza kuwa na hasira kama mbogo, why anatetea nafasi yake kuporwa, nafasi ipi nafasi ya kunyimwa heshima yake.
Ukiona unakaa na mkaka mwezi mmoja ghafla anapotea kimya kimya, chunguza maneno yako kwake, huyo siyo mdada mwenzako ujue, unamzodoa amekuwa mdogo wako? amekuwa mdada mwenzako? silaha ya mwanamke mwenye akili ya kulinda nyumba yake yuko makini sana katika kufungua kinywa chake.

Hata kama Yesu kaongea na wewe mengi juu yako katika mahusiano yako, unahitaji nidhamu sana katika kuongea nae, wengi wameachwa kwa ajili ya dharau na kiburi, mdada yeyote mwenye kiburi chunguza mwisho wake, ni kuachika kila kukicha
Ndiyo maana unaweza kuona wakaka wengi waliookoka utakuta wanammendea mdada mmoja kwenye fellowship, why, kitu gani wameona, ​HESHIMA​ ukiona wakaka hawakatizi kwako cha kwanza omba Mungu aondoe mtazamo wanaouona juu yako ya kiburi ili akupe hekima inayoleta nidhamu ya heshima kwa mkaka, huamini endelea na kiburi chako uone kama kuna mkaka atapata shauku ya kuwa na wewe.

Mungu awabariki sana wadada wote wenye heshima, mjue uzuri ni ubatili bali mwanamke amchaye Bwana huyo ndiye atakayesifiwa .
Somo ni refu, sijaanza kufundisha hapo, huo ni utangulizi tu.
Chuoni huwa tunauliza watu waliotutangulia juu ya taarifa muhimu za mwl, nini huyo mwl anataka, je huwa anatabia za kubana course work? je anapenda uandike sana maelezo? au hataki maelezo sana? je anatoaga mekapu? yote hiyo ni ili kuenda naye vizuri baada ya kumfahamu, ninachohofia wengi hukumbuka shuka wakati wa asubuhi, means TOO LATE, fahamu sana mambo ambayo mkaka anayahitaji, mkaka mbona utafurahia tuuu? yajue tu, leo nimeongelea point moja tu. Nitawaletea point wakati mwingine poin nyingine .

HIZI NDIO SABABU KUMI KWANINI UACHE KUNYWA SODA KWANZIA LEO.

HIZI NDIO SABABU KUMI KWANINI UACHE KUNYWA SODA KWANZIA LEO.
👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻

Inawezekana una bahati sana kuiona hii makala na itakujenga sana kiafya...tafiti zinasema kwamba mtu mmoja anayekunywa soda moja kwa siku, anakunywa zaidi ya galoni au dumu 56 za soda kwa
mwaka.
Japokua kuna watu wamekiri kunywa hata zaidi ya soda moja kwa siku ambayo huenda wanakunywa zaidi ya hicho kipimo.
Biashara ya soda inalipa sana duniani kwani ni kinywaji cha pili
kinachoongoza kunywewa duniani baada ya maji.
Sasa ukiangalia mahusiano ya unywaji mdogo wa soda kila siku kiafya una madhara makubwa kuliko unywaji mdogo wa pombe kila
siku.
Yaani ni bora unywe chupa moja ya bia kila siku kuliko chupa moja ya soda kila siku.

Yafuatayo ni madhara ya soda ambayo yatakufanya ufikirie mara mbili kunywa soda tena.

1.Ugonjwa wa kisukari;

Kunywa soda moja ni sawa na kunywa vijiko 10 vya sukari, baada ya kunywa sukari hupanda sana mwilini na kongosho hutoa homoni ya insulini nyingi ili kushusha sukari.
Muda unavyozidi kwenda insulini huendelea kuishiwa nguvu[insulin resisitance] na hali hii husababisha kisukari.

2. Unene na kitambi;

Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Havard umegundua kwamba watu wanaokunywa soda hunenepa mara mbili zaidi ya wale ambao hawanywi hivyo kama uko busy unapunguza uzito na pia mnywaji wa soda basi unapoteza muda.

3. Upungufu wa madini muhimu mwilini;

Soda ina kemikali inayoitwa phosporic acid ambayo huzuia mwili kuchukua madini ya calcium kwenye chakula ambayo ni muhimu sana kwa ajili ya mifupa na misuli yenye afya kweye mwili wa binadamu.

4. Ugonjwa wa kansa;

Soda ina kemikali inayoitwa caffeine ambayo imehusishwa na cancer mbalimbali za mwili mfano kansa ya kongosho, kansa ya utumbo na magonjwa mengine kama presha ya damu na kansa ya matiti.

5. Huongeza sumu mwilini;

Soda haina lishe wala faida yeyote ile kwenye mwili wa binadamu hivyo huongeza kiasi kikubwa cha sumu mwilini ambacho ni hatari sana kwa afya mtumiaji.
Sumu hizo huongeza hatari ya kupata ugonjwa wa presha, na kuua figo.

6. Hubadilisha rangi ya meno;

Kila mtu anataka kuwa na meno masafi na meupe lakini baadhi ya soda zina kiasi kikubwa cha tindikali ambacho hushambulia na kuharibu meno kwa muda mfupi hivyo kama unasumbuliwa na meno basi huu ni muda mzuri wa kuachana nayo.

7. Addiction;

Soda nyingi zina tabia ya kumfanya mtu apate ulevi wa soda husika yaani kuna watu unakuta anapenda sana soda fulani na asipoinywa kwa siku atahisi kama amepungukiwa kabisa na kitu fulani mwilini.
Hii itakufanya uwe mtumwa wa mwili wako mwenyewe.

8. Huongeza kasi ya uzee;

Sumu ambazo unazipokea kwenye soda zinazeesha mtu mapema sana yani kijana mdogo wa miaka 20 hujikuta anaonekana kama miaka 35.

9. Hupunguza sana maji mwilini ;

Soda ina kiwango kikubwa cha madini ya sodium ambayo humfanya mtu abaki na maji kidogo na kwa muda mrefu atapata matatizo mengine ya kiafya kama mawe ya kwenye figo[kidney stone] na mawe kwenye nyongo ya binadamu.

10.Mwisho;

Ni vizuri kubadili mfumo wako wa maisha na kuanza kunywa vitu ambavyo haviharibu mwili yaani badala ya kunywa soda basi tumia juice (unayoitengeneza mwenyewe) ambayo ni mbadala mkubwa wa soda, lakini pia unaweza kunywa maziwa na kadhalika.

  RATIBA NGUMU NI NYEPESIKWA MAFANIKIO

              RATIBA NGUMU NI NYEPESI
       KWA MAFANIKIO.

Ni rahisi kusikia watu wanasema jamaa anaratiba ngumu au pamoja na ratiba yake lakini bado amekuja na huku au bado amefanya na hili. Wanasahau  kuwa ratiba ngumu ni nyepesi kwa mafanikio na ratiba nyepesi ni ngumu kwa mafanikio. Tunatofautiana sana katika ratiba zetu kutokana na utofauti wa maono na vipaumbele vyetu. Wakati wengine wanatafuta vitu vya kufanya lakini wengine kupata muda wa kupumzika ni muujiza. Na ukitaka kukorofishana nao ingilia muda wao wa kupumzika. Maana wanauheshimu.

Unapatikana kiurahisi kwa sababu huna cha kufanya ratiba yako ni nyepesi sana na inawezekana pia huna wewe ni bora siku iende ulale uamke. Cha ajabu wengi tunapenda mafanikio lakini gharama za mafanikio hatutaki kuzilipa. Kila siku watu wanakukuta katika kijiwe na wanakuacha. Haujui ni siku ipi kwako imebana na siku ipi una angalau nafasi. Siku zote kwako sawa.
-Ratiba ngumu sio ile ya kubandika ukutani na kubaki unaitazama.
-Ratiba ngumu sio ile haupatikani na unachokifanya hakionekani kwako wala kwa waliokuzunguka.
-Ratiba ngumu sio ile unakosa hata muda na familia yako.
-Ratiba ngumu sio ile unakosa hata muda wa kuingia nyumba za ibada.
-Ratiba ngumu sio ile unakosa hata muda wa kupumzika.
-Ratiba ngumu sio ile unakosa hata muda wa kula bata na rafiki zako.
-Ratiba ngumu inajumuisha yote hayo niliyotaja pamoja na kuacha alama kwa jamii yako kwa yale unayoyafanya.

Mafanikio mengi ni matokeo ya jitihada na bidii kubwa katika yale mtu anafanya. Jitihada hizo ndizo zinampelekea kuwa na ratiba ambayo akiifuta na kufanya kazi kwa bidii inayotakiwa itamletea mafanikio aliyotarajia kuyapata au kuyafikia. Akili inaposhughulishwa na mambo mengi yaliyopangiliwa inakuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri na kutatua mambo. Ndio sababu waingereza wanamsemo wao wanasema ' ukitaka jambo lako lifanywe haraka na kufanikiwa mpe mtu busy kuliko wote alifanye' wanaamini hivyo sababu wanaamini atafanya haraka ili aweze kuendelea na mambo yake lakini atalifanya vizuri ili asije ambiwa kurudia kulifanya maana atakuwa anapoteza muda kurudia kufanya jambo hilo.
Ikague ratiba yako ni nyepesi au ngumu. Je itakufanya ufanikiwe katika malengo uliyojiwekea. Ukiona ratiba yako imebana lakini nje ya malengo uliyojiwekea ujue siyo ratiba ngumu hiyo. Ni nyepesi sana.

#Kila kitu kinatengenezwa#
JIFUNZE KUJIFUNZA
@Kuwa Ni Kufanya&

TIBA NA USHAURI WA MTU MWENYE VIDONDA VYA TUMBO

TIBA NA USHAURI WA MTU MWENYE VIDONDA VYA TUMBO

Dawa ya Vidonda vya Tumbo MAANDALIZI;

-Chukua karoti kilo1 ponda iwe laini na kisha uchemshe kwa dakika 15 ndani ya maji lita 1 na nusu au mbili chuja,kunywa juisi yake kwa kutibu vidonda tumbo au saratani ya tumbo,saratani ya kizazi tumia nusu kikombe cha chai miezi 3 mpaka 6. Dawa ingine ya Vidond vya tumbo Vidonda tumbo:
Kula kipande cha papai kisichoiva vizuri kila siku alfajiri, ukimaliza shushia na mbegu moja tu ya kitunguu swaumu. Hakikisha unazidisha kiwango cha kunywa maji siku zote utakazo jitibia vidonda hivyo, na ikifika siku 13 hadi 16 utanipigia simu kunitaarifu kuwa vidonda vimepona.
Kama kipato chako ni kidogo na kupata papai kila siku ni gharama, basi usikonde. Chuma majani mawili ya mpapai kisha katakata kama mboga ya kupikwa, tia katika chupa kubwa ya lita mbili za maji na kunywa kutwa nzima kidogo kidogo hadi yaishe. Waweza kutia vipande vya mapapai machanga yaliyokatwakatwa pia badala ya majani. VYAKULA
TIBA KWA WAGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO
Ili kupunguza makali au kujiepusha kabisa na ugonjwa wa vidonda vya tumbo, unapaswa kujiepusha na tabia ya kula na kushiba kupita kiasi, kwa sababu kushiba sana huchochea uzalishaji wa asidi nyingi wakati wa usagaji chakula tumboni.
Mbali na hilo, vyakula vyenye mafuta na sukari nyingi na vyenye kiwango kidogo sana cha kamba lishe, imethibitika kuwa husababisha madhara mengi tumboni. Katika makala ya leo, tutaangalia aina ya vyakula anavyopaswa kula au kuviepuka mgonjwa ili kupata nafuu na kuishi bila kusumbuliwa nao:

VYAKULA VYENYE VIUNGO VINGI
Epuka ulaji wa vyakula vilivyopikwa na kuungwa viungo vingi vya aina mbalimbali, kama vile pilipili kali za aina zote na viungo vingine vyenye ladha ya ukali ambavyo hutiwa ndani ya mboga ama chakula ili kuongeza ladha.

POMBE NA KAHAWA
Pombe na kahawa au vinywaji vingine vyenye ‘caffeine’, vinaweza kuleta matatizo kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo na kwa mtu asiye navyo anaweza kupatwa na tatizo, hivyo ni vyema kuepuka au kutumia kwa kiasi kidogo vinywaji hivi. Kimsingi vinywaji hivi huongeza asidi tumboni na hivyo vinaweza kusababisha vidonda au kuzidisha maumivu kwa anayeumwa.

ULAJI CHUMVI
Utafiti uliowahi kufanywa nchini Marekani umeonesha kuwepo kwa uhusiano kati ya ulaji chumvi na vidonda vya tumbo. Mgonjwa anashauriwa kuepuka ulaji wa vyakula vyenye chumvi nyingi, hususan vyakula vya kusindika ambavyo huwekwa chumvi nyingi ili visiharibike haraka. Pia jiepushe na kuongeza chumvi kwenye sahani wakati wa kula.

MAFUTA YA SAMAKI
Baadhi ya utafiti unashauri wagonjwa wa vidonda vya tumbo wale mafuta yatokanayo na samaki (Omega-3 fats) ambayo yameonekana kutoa ahueni kwa wagonjwa. Na kwa mtu ambaye si mgonjwa atakuwa anajiwekea kinga dhidi ya vidonda vya tumbo na magonjwa mengine ya tumbo.

VITAMINI NA MADINI
Ulaji wa vyakula vyenye madini na vitamini kwa wingi husaidia sana kuleta ahueni kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo na kutoa kinga kwa wale ambao hawajaathirika. Wataalamu wa lishe wanashauri kupenda kula matunda na mboga za majani kama vile karoti, juisi ya kabeji, ndizi mbivu, na matunda mengine yenye vitamin C, halikadhalika maziwa ya mbuzi, jibini na cream za maziwa huleta ahueni.

STAILI YA MAISHA NA VIDONDA VYA TUMBO
Licha ya kusabisha Saratani, uvutaji sigara pia huongeza hatari ya mtu kupatwa na ugonjwa wa vidonda vya tumbo, hivyo ni sababu tosha ya kuacha uvutaji sigareti. Japo msongo wa mawazo unaweza kuwa vigumu kuuhusisha moja kwa moja na vidonda vya tumbo, lakini maisha ya wasiwasi, ukichangaya na ulaji mbovu, huweza kusababisha ugonjwa huu, hivyo kama unataka kujiepusha au kupunguza makali ya ugonjwa huu, ni muhimu kuzingatia ulaji sahihi na kuishi maisha ya furaha.

UKWELI JUU YA MAMBO AMBAYO MWANAMKE ANAYAHITAJI TOKA KWA MWANAUME.

UKWELI JUU YA MAMBO AMBAYO MWANAMKE ANAYAHITAJI.

Bwana Yesu Asifiwe, moja ya mambo yanayoleta shida kwa wakaka wengi ni kushindwa kujua ya kwamba kibiblia kuna vitu vya msingi ambavyo wadada wanavihitaji maana yake ni vya kwao by nature and you cannot separate it from them, it's unique designed.

Suala la kuokoka haliondoa kile ambacho mdada anakihitaji isipokuwa linaboresha lile jambo ambalo shetani aliharibu baada ya anguko, hivyo tunategemea mtu anapookoka atasimama ipasavyo katika kujua mambo ambayo mdada anayahitaji, jambo hili kwa wadada wengi hawaliona nakujikuta wengi mahusiano yao yakiharibika kwa sababu wakaka wengi waliookoka wanahisi kila kitu duniani ni maombi tu

1. Wadada wanahitaji upendo wa dhati, means kupendwa, hii ndiyo raha yao, muda wote shauku yao, waone mtu aliyepotayari kupenda, why wanajiona ya kuwa wapo salama kabisa and protected, jambo ambalo wakaka wengi huhisi wapo kimwili, ninakuhakikishia kama upo kwenye mahusiano na mdada huonyeshi kumpenda kwa dhati, ni vyepesi mdada huyo huyo ukamkuta tayari haupo ndani ya moyo wake kwa sababu anakuona haupo serious kwake.

Mdada katika maisha yake yote hutasikia akilalamika ya kwamba mkaka hamuheshimu isipokuwa utakuta akilalamika yakwamba hapendwi.

Na mkaka case yake kubwa hutakuta akilalamika yakwamba hapendwi isipokuwa utakuta analalamika yakwamba haheshimiwi

Ni vizuri kujua uhitaji wa kila pande, hata kama ni ngumu kumeza jitahid tu kujifunza itakusaidia.

2. Wadada wanahitaji sana mawasiliano na kuzungumzishwa, yaani ni hatari sana, katika uchunguzi wangu wakaka wengi si wazungumzaji, asilimia kubwa si wazungumzaji kabisa, lakini mdada anakifeel vzr akizungumzishwa, mawasiliano, na hii imekuwa ni vita kwa wakaka wako busy na huduma🙈, hawana tyme hata ya kuwasemesha wadada, muda wote ni prayer, Bwana Yesu asifiwe mama, umesoma Yeremia, wakimaliza hapo ndiyo kamaliza, mim nakueleza utaachwa saa tatu kamili asubuhi, maandiko yanasema tukae nao kwa akili, means lakiza ujitahidi kujua nini wanahitaji.

3.Mdada ni ngumu kuweka mambo na kuyatunza moyoni mwake sana ndiyo maana akiyasema anakuwa huru ndani ya moyo wake tofauti na mkaka ambaye yupo tayari kukaa nayo kwa muda mrefu, ni muwazi siku zote na asilimia kubwa ni waaminifu, msinikasirikie wakaka😊

Kwani ukimuita jina zuri utachubuka? upako utaisha? mnatia aibu sana🙈, ndiyo maana mkaka kumwambia umependeza haoni chochote, mwambie mdada uone, ina add value kubwa sanaa..

4. Urafiki, Kiwango kikubwa cha mahusiano mazuri ni urafiki, hiki ni kiwango ambacho mdada anakihitaji sana, mambo yake anayopitia wakwanza kujua awe mkaka anayetegemea kuwa mume wake, hata kama umeoa na kuolewa tayari mnahitaji kumentain urafiki, Isaka na Rebecca walikuwa marafiki kitu ambacho kilipelekea Mfame kujua ya kuwa siyo dada yake baada ya kuwaona wakicheza cheza, unadhani walikuwa wanacheza rede, mdako au kombolela? The highest Relationship is built into friendship 😋

5. Shauku ya kuuliza maswali, wanapenda sana kuuliza uliza maswali mengi, means wanataka kuelewa zaidi, awe na uhakika, jambo linalowakera sana wakaka wengi maana hawataki kuulizwa ulizwa maswali.

Hii ndiyo furaha yao, kuuliza maswali pale jambo linapoonekana kutoeleweka vzr kwao, ila kwa wakaka wengi huwa siyo watu wa kuuliza uliza maswali mengi kama wadada, hivyo tuwaelewe tu ndivyo walivyoumbwa.

Sasa wadada wengi hata kama wanauliza maswali mengi lakini hawajui kwa nini wao asili yao hujikuta wakiuliza maswali mengi kwa wakaka kiasi kwamba wakaka wengi wamewaogopa wadada kwa sababu ya maswali yao.

Kadharika na wakaka nao hawajui kwa nini wanaulizwa  maswali mengi

Jibu ni hili, Mungu alimpatia Adamu maelekezo ya namna ya kuishi katika bustani ya Edeni, na hayo maelezo Adam akamueleza Eva, hivyo Eda kuuliza maswali ni kutaka kujiridhisha juu ya maelezo aliyopewa Adam na Mungu, kumbuka ukiona mdada anakuuliza maswali mengi ni kwa ajili ya usalama wako ila mpaka awe mdada mwenye hofu ya Mungu vinginevyo atachuma matunda uliyokatazwa na utakula tu

Si vyepesi sana kujua hili suala kwa urahisi, lakini pia ni muhimu sana kufahamu haya mambo itakusaidia mbele ya safari

Wakaka wengi wanakuwa bored wanapoulizwa ulizwa maswali 😅, shida ni nini mpaka unakasirika ukibanwa maswali? ndiyo raha yao ujue

Kuna vitu ukiwa rafiki na mdada hautavikuta kwa Mchungaji wako kanisani, urafiki hauna mipaka maana yake atakuwa huru kukueleza

6. Mdada yeyote anashauku ya kusapotiwa kifedha ndani ya moyo wake, hii inaweza isiwe issue kubwa sana kwa wadada wanaofanya kaz, but Mungu alimuweka Adam kwenye bustan ya Eden ili aitunze na kuwa provider kwa familia yake, yes sikushauri hata kidogo mkaka uoe kama huna pesa.

7. Wanapenda sana mtu wa kujitoa katika mambo ya kifamilia, na muda mrefu atakuuliza mambo ya maendeleo ya kifamilia

8. Mdada anatamani kumfuata kiongozi wa familia, mara nyingi hata kama anajua jambo hutamani kujua leader au head of the family anasemaje, sasa mahead of the family wengi hawajitambui hata kidogo wanahisi ubabe ni dawa.

Monday, January 15, 2018

MAMBO 7 MUHIMU KWANINI UWE NA MWANAMKE BORA NA SI BORA MWANAMKE..

Kwangu mimi nilipata msukumo wa kuandika walaka huu baada ya kipindi ambacho kilinivutia sana ni kipindi cha kampeni za uchaguzi nchini Marekani.

Ni pale Obama akiwa katika kampeni kwenye moja ya majimbo kugombea duru ya pili ya uraisi aliposimamisha hotuba yake na kutambua uwepo wa mkewe Michelle.
Obama alisema, "Mke wangu amekuwa bega kwa bega na mimi tokea niko chuo, kuna kipindi nilishindwa kulipa ada ila yeye ndiye aliyenilipia"

Obama akaenda mbali zaidi na kukiri mbele ya jamii ya kimataifa kwamba asingekuwepo hapo alipo kama sio mke wake Michelle.
Hivyo basi, nashauri kwamba mwanamke ambae mwanaume atakua nae huenda akawa chachu ya mafanikio na baraka kwake au anaweza akamrudisha nyuma kabisa katika mipango yake.

SASA ZIFUATAZO NDIO SABABU NLIZOONA KUU SABA ZA MUHIMU KWANINI MWANAUME LAZIMA UPATE MWANAMKE BORA NA SAHIHI...

√1. Kila mwanamke anao uwezo wa kukuridhisha kimapenzi ila mwanamke sahihi na bora pekee ndiue anaeweza kuku-challenge kiakili na kuwa 'intellectually inspired'.

2. Mwanamke yeyote anaweza kukuteka kihisia, ila yule sahihi pekee ndiye mwenye uwezo wa kukuteka kiroho na ukamtumikia Mungu wako.

3. Mwanamke yeyote anaweza akakushawishi muandike mpango wa harusi (wedding plan), ila mwanamke sahihi peke yake ndie mwenye uwezo wa kukuandikia na kukushauri mpango wa biashara (Business plan).

4. Kila mwanamke anaweza akakubusu tena 'French kiss' ila mwanamke bora pekee ndio mwenye uwezo wa kukutamkia maneno yaliyojaa busara na hekima.

√5. Kila mwanamke anaweza akakupenda sana tu tena kama una pesa, ila mwanamke aliye bora pekee ndiye anaeweza kusimama na wewe hata kukuinua pale utakapokuwa huna kitu.

√6. Mwanamke yeyote anao uwezo wa kukushibisha kwa kukupikia chakula kitamu, ila mwanamke bora pekee ndio mwenye uwezo wa kukulisha chakula cha ubongo.

7. Kila mwanamke anao uwezo wa kukushawishi chumbani ila mwanamke bora pekee ndio mwenye uwezo wa kukushawishi umrudie Mungu wako.

Mwisho ngoja nihitimishe kwa kusema hivi ukisoma vitabu vya kihistoria kuhusu Winstom Churchhill mpaka Abraham Lincoln, na kutoka kwa Nelson Mandela mpaka kwa Martin Luther King Jr lao moja kwamba “No matter how strong a Man is, he is only as strong as the Woman he marries” Kwa tafsiri yangu ya kuunga unga isiyo sahihi sana Wanamaanisha "haijalishi ni kwa kiasi gani mwanaume una nguvu, nguvu zako zina athiriwa kwa kiasi kikubwa na mwanamke utakaemuoa"