MWANGA UMEBEBA HATIMA YA MAISHA YAKO!!
•
•
Mwanga hata siku moja huwa hauwezi kushindana na giza.Mwanga una uwezo mkubwa sana kiasi kwamba giza haliwezi kuwa competitor wake. Popote penye giza mwanga ukitokea tu basi giza linakimbia haraka sana na kwenda mbali au kuondoka kabisa.
•
Adui wa kwanza kabisa wa Mafanikio ya mwanadamu ni giza lililopo ndani yake. Kukosa maarifa na taarifa sahihi ni kuwa na giza totoro ndani yako.
•
Mafanikio ya mtu yeyote huanzia kwa kuwa na mwanga kwanza kwenye maisha yake.Huwezi kuona chochote gizani. Huwezi kufanya shughuli yoyote gizani. Huwezi kula, huwezi kusoma,huwezi kuandika, kuwezi kuchukua kitu chochote kirahisi ukiwa gizani. Hata ukiwekewa zawadi kubwa kiasi gani kukiwa na giza huwezi kuona hiyo zawadi.
•
Mtu anapopata taarifa sahihi na maarifa kuhusu jambo fulani hiyo ndo huwa hatua ya kwanza kabisa ya mafanikio ya huyo mtu kupata alichokuwa anakitaka na mtu akipata maarifa tunasema mwanga umeingia ndani yake na hivyo giza limekimbia. Tunapozungumzia mwanga tunazungumzia kuzitafuta taarifa na maarifa zitakazoondoa giza la ujinga uliopo akilini mwako.
•
Kukosa maarifa na taarifa chanya kumesababisha masikini wengi duniani kuliko kingine chochote. Vijana wanalalamika hakuna fursa ni kwasababu wana giza ndani yao. Vijana wanalalamika vyuma vimekaza ni kwasababu hawana mwanga ndani yao.
•
Warren Buffet anasema ukiwa na maarifa na taarifa sahihi ni mwanzo wa wewe kufanikiwa kwani maarifa yanaleta mtaji, maarifa yanaleta mbinu, maarifa yanaleta wateja, maarifa yanavuta fursa, maarifa yanatenegeneza network sahihi. Maarifa yanakuepusha na hasara na kuingizwa mkenge, maarifa yatakuketisha na wakuu, maarifa ndo yatakufanya uvumilie unapopita kipindi cha magumu, maarifa yatakufanya upambane kwa bidii na kujituma.
•
Kumbuka maandiko matakatifu yanasema "Tunaangamia kwa kukosa maarifa". Kwa maana harisi ni kuwa, watu wanakuwa masikini kwa kukosa maarifa. Watu wanafeli kwenye ndoto zao kwa kukosa maarifa. Watu wanakata tamaa za ndoto zao kwa kukosa maarifa. Kwa kifupi ni kuwa MAARIFA NDO YAMESABABISHA WATU KUFANIKIWA NA WATU KUFELI.
•
Live Your Dream!!
•
Mungu Ibariki Tanzania
Tuesday, April 9, 2019
MWANGA UMEBEBA HATIMA YA MAISHA YAKO!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment