Friday, May 10, 2019
Watu sikuhizi wanaacha kufanya ya kwao wanaanza kujadili na kuhukumu maisha ya wengine,utasikia......flani kajiachia sana sikuhizi,flani ni mbea,flani kashinda njaa,flani kabakwa,flani kaachwaa,flani kaibaa,flani sio mwaminifu,flani amekuwa mlevi,flani amebadirika,flani anafanya dhambi kila siku,mambo meeengi ya watu wengine unaacha kutimiza mambo yako, rafiki yangu this world is not our home!
Huu ulimwengu si nyumbani kwetu kila mtu atakufa na kifurushi chake na atatoa hesabu ya kifurushi chake yeye mwenyewe unapata wapi ujasiri wa kumsema na kumuhukumu mwingine??? Deal na Maisha Yako rafiki!
Una mambo mengi sana ya kufanya ili kutimiza kusudi la wewe kuwepo hapa duniani,wala hujafika hata nusu ya makusudio unapata wapi muda wa kufatilia mambo ya watu???
No matter flani kafanya nn,wewe haikuhusu ilihali haina mashiko kwenye assignment yako basi pambana na kusudi lako, usimseme mtu wala usimfatilie mtu,kumbuka kila mtu anamapungufu yake hivyo hata wewe una yakwako,so pambana nayo.
Mungu ndiye ajuaye maisha ya kila mmoja wetu,acha kukosoa maisha ya wengine pambana kuweka sawa safari ya maisha ya kwako, mengine Mungu atadeal nayo.
Umekaa kila siku mambo yako hayaendi kazi unaongea ya watu tu,tena bora ingekua unaongea kwa wema unaeneza mabaya tu kila siku huchoki???
Tukitafuta la kwako jema hata moja tutalipata???
Huu mwaka hebu badilika basi,achana na maisha ya watu hebu litafute kusudi lako pambana nalo mpaka litimie, watu hawabadilishwi kwa maneno yako bali kwa matendo yako,
Ukifanya vyema kwenye kusudi lako na ukawa mwaminifu huwezi jua unaweza kuwagusa na wengine wakabadilika kuliko kushinda unaongea mambo ya mtu mwingine,kwanza hawezi kukuelewa.......unamwambia mtu afunge kusali wakati wewe hujawahi hata kufunga siku moja, unamwambia mtu aache ulevi huku na wewe unapiga vyombo??
Flani amekengeuka,basi muombee maisha yaendelee,Kijana mwenzako katoka nje ya line muombee maisha yaendelee!
Tujifunze kutafuta kutimiza assignment zetu zilizofanya tukaja kuishi hapa duniani..
Tuesday, April 9, 2019
MWANGA UMEBEBA HATIMA YA MAISHA YAKO!!
MWANGA UMEBEBA HATIMA YA MAISHA YAKO!!
•
•
Mwanga hata siku moja huwa hauwezi kushindana na giza.Mwanga una uwezo mkubwa sana kiasi kwamba giza haliwezi kuwa competitor wake. Popote penye giza mwanga ukitokea tu basi giza linakimbia haraka sana na kwenda mbali au kuondoka kabisa.
•
Adui wa kwanza kabisa wa Mafanikio ya mwanadamu ni giza lililopo ndani yake. Kukosa maarifa na taarifa sahihi ni kuwa na giza totoro ndani yako.
•
Mafanikio ya mtu yeyote huanzia kwa kuwa na mwanga kwanza kwenye maisha yake.Huwezi kuona chochote gizani. Huwezi kufanya shughuli yoyote gizani. Huwezi kula, huwezi kusoma,huwezi kuandika, kuwezi kuchukua kitu chochote kirahisi ukiwa gizani. Hata ukiwekewa zawadi kubwa kiasi gani kukiwa na giza huwezi kuona hiyo zawadi.
•
Mtu anapopata taarifa sahihi na maarifa kuhusu jambo fulani hiyo ndo huwa hatua ya kwanza kabisa ya mafanikio ya huyo mtu kupata alichokuwa anakitaka na mtu akipata maarifa tunasema mwanga umeingia ndani yake na hivyo giza limekimbia. Tunapozungumzia mwanga tunazungumzia kuzitafuta taarifa na maarifa zitakazoondoa giza la ujinga uliopo akilini mwako.
•
Kukosa maarifa na taarifa chanya kumesababisha masikini wengi duniani kuliko kingine chochote. Vijana wanalalamika hakuna fursa ni kwasababu wana giza ndani yao. Vijana wanalalamika vyuma vimekaza ni kwasababu hawana mwanga ndani yao.
•
Warren Buffet anasema ukiwa na maarifa na taarifa sahihi ni mwanzo wa wewe kufanikiwa kwani maarifa yanaleta mtaji, maarifa yanaleta mbinu, maarifa yanaleta wateja, maarifa yanavuta fursa, maarifa yanatenegeneza network sahihi. Maarifa yanakuepusha na hasara na kuingizwa mkenge, maarifa yatakuketisha na wakuu, maarifa ndo yatakufanya uvumilie unapopita kipindi cha magumu, maarifa yatakufanya upambane kwa bidii na kujituma.
•
Kumbuka maandiko matakatifu yanasema "Tunaangamia kwa kukosa maarifa". Kwa maana harisi ni kuwa, watu wanakuwa masikini kwa kukosa maarifa. Watu wanafeli kwenye ndoto zao kwa kukosa maarifa. Watu wanakata tamaa za ndoto zao kwa kukosa maarifa. Kwa kifupi ni kuwa MAARIFA NDO YAMESABABISHA WATU KUFANIKIWA NA WATU KUFELI.
•
Live Your Dream!!
•
Mungu Ibariki Tanzania