Kitu kimoja kati ya vitu vya muhimu sana katika ulimwengu huu ni
kujifunza kudeal na assignment yako ya wewe kuishi hapa duniani basi!
Watu sikuhizi wanaacha kufanya ya kwao wanaanza kujadili na kuhukumu
maisha ya wengine,utasikia......flani kajiachia sana sikuhizi,flani ni
mbea,flani kashinda njaa,flani kabakwa,flani kaachwaa,flani kaibaa,flani
sio mwaminifu,flani amekuwa mlevi,flani amebadirika,flani anafanya
dhambi kila siku,mambo meeengi ya watu wengine unaacha kutimiza mambo yako, rafiki yangu this world is not our home!
Huu ulimwengu si nyumbani kwetu kila mtu atakufa na kifurushi chake na
atatoa hesabu ya kifurushi chake yeye mwenyewe unapata wapi ujasiri wa
kumsema na kumuhukumu mwingine??? Deal na Maisha Yako rafiki!
Una mambo mengi sana ya kufanya ili kutimiza kusudi la wewe kuwepo hapa
duniani,wala hujafika hata nusu ya makusudio unapata wapi muda wa
kufatilia mambo ya watu???
No matter flani kafanya nn,wewe
haikuhusu ilihali haina mashiko kwenye assignment yako basi pambana na
kusudi lako, usimseme mtu wala usimfatilie mtu,kumbuka kila mtu
anamapungufu yake hivyo hata wewe una yakwako,so pambana nayo.
Mungu ndiye ajuaye maisha ya kila mmoja wetu,acha kukosoa maisha ya
wengine pambana kuweka sawa safari ya maisha ya kwako, mengine Mungu
atadeal nayo.
Umekaa kila siku mambo yako hayaendi kazi unaongea
ya watu tu,tena bora ingekua unaongea kwa wema unaeneza mabaya tu kila
siku huchoki???
Tukitafuta la kwako jema hata moja tutalipata???
Huu mwaka hebu badilika basi,achana na maisha ya watu hebu litafute
kusudi lako pambana nalo mpaka litimie, watu hawabadilishwi kwa maneno
yako bali kwa matendo yako,
Ukifanya vyema kwenye kusudi lako na
ukawa mwaminifu huwezi jua unaweza kuwagusa na wengine wakabadilika
kuliko kushinda unaongea mambo ya mtu mwingine,kwanza hawezi
kukuelewa.......unamwambia mtu afunge kusali wakati wewe hujawahi hata
kufunga siku moja, unamwambia mtu aache ulevi huku na wewe unapiga
vyombo??
Flani amekengeuka,basi muombee maisha yaendelee,Kijana mwenzako katoka nje ya line muombee maisha yaendelee!
Tujifunze kutafuta kutimiza assignment zetu zilizofanya tukaja kuishi hapa duniani..